Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 8/07 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—2007
  • Habari Zinazolingana
  • Imani ya Mtoto
    Amkeni!—2006
  • Maumbo Yanayovutia ya Mimea
    Amkeni!—2006
  • Walijitoa Wenyewe kwa Hiari—Nchini Mexico
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Yesu Alisema Tunapaswa Kuwatendeaje Wengine?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2007
g 8/07 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Imani ya Mtoto (Agosti 2006) Ninatazamia kumwona Dustin, na mamilioni ya wengine ambao wamekufa, wakikimbia na kuruka wakiwa na nguvu za ujana kwenye ulimwengu mpya ambao uko karibu sana.

A. A., Sri Lanka

Imani na ujasiri wa Dustin ulinigusa moyo sana. Simulizi lake limenisaidia kuthamini kweli katika maisha yangu na kujiwekea miradi inayofaa. Sasa ninatambua ninapaswa kutanguliza uhusiano wangu na Yehova na mambo ya Ufalme maishani.

M.C.V., Brazili

Moyo wangu uliguswa sana na jinsi Dustin alivyothamini sana kweli. Matendo yake yalionyesha kwamba alitaka kumpendeza Yehova na kuwatumikia wengine. Kama Dustin, mimi pia ninataka ‘kukimbia mwendo mpaka mwisho, na kushika imani’!

M. N., Japani

Nina umri wa miaka saba. Asanteni sana kwa kuchapisha simulizi hilo. Nilivutiwa sana na jinsi Dustin alivyokuwa na imani yenye nguvu katika Yehova, ingawa alikuwa na ugonjwa mbaya. Mfano wake umenichochea kufanya mengi katika utumishi wa Mungu.

T. D., Italia

Maumbo Yanayovutia ya Mimea (Septemba 2006) Nilichunguza makala hiyo kwa saa moja na nusu! Ilikuwa yenye kuelimisha sana! Nilichora michoro ili niweze kuielewa vizuri. Hata hivyo, pembenukta ya 13/21 haifafanui uwiano wa pembenukta bora ya mzunguko, lakini inafafanua zaidi sehemu inayobaki ya digrii 222.5.

L. C., Marekani

“Amkeni!” linajibu: Wasomaji wengi wameonyesha kwa usahihi kwamba uwiano wa pembenukta bora ni karibu digrii 222.5. Lakini kwa nini makala yetu ilisema pembenukta bora ni digrii 137.5, yaani, pembe hiyohiyo inapopimwa kinyume? Chanzo kimoja kutoka katika Intaneti kiitwacho “Web resource MathWorld” kinasema: “Pembenukta bora ni ile inayoweza kugawanya umbo kamili, yaani lenye digrii 360, kwa kiwango kilicho sawa (lakini inapimwa kinyume hivi kwamba inapungua digrii 180).” Akifafanua kwa nini wanahisabati na wanasayansi wanaelezea pembenukta bora kwa njia hiyo, mwanahisabati Mwingereza Dakt. Ron Knott anasema: “Kwa kawaida sisi ‘huona’ tu ile pembe ndogo.” Hivyo, hata ingawa pembenukta bora ina uwiano wa 13/21 (yaani zaidi ya nusu), kwa kawaida pembenukia bora inaonyeshwa kuwa digrii 137.5 (yaani inapungua nusu).

“Wafungwa kwa Sababu ya Imani Yao” (Aprili 2006) Mimi si Shahidi wa Yehova, lakini hilo halinifanyi nisiwaheshimu waumini wenzenu. Nilikutana na Mashahidi wa Yehova kadhaa nilipokuwa nikitumikia kifungo kwenye kambi ya mateso ya Gross-Rosen na Buchenwald. Tabia zao zilikuwa nzuri na imani yao thabiti hivi kwamba waliheshimiwa na kustaajabiwa na wafungwa wengine wote. Hata askari wa Hitler walivutiwa nao. Mashahidi wa Yehova wanakaribishwa wakati wowote nyumbani kwangu.

P. V., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki