Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/11 kur. 15-31
  • Mazungumzo Ya Familia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mazungumzo Ya Familia
  • Amkeni!—2011
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?
  • Kusanya na Ujifunze
  • Watu na Nchi
  • Watoto Watafute Picha
  • MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31
  • Alitenda kwa Hekima, Ujasiri, na Bila Ubinafsi
    Igeni Imani Yao
  • Alitenda kwa Hekima, Ujasiri, na Bila Ubinafsi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Aliwatetea Watu wa Mungu
    Igeni Imani Yao
  • Aliwatetea Watu wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 4/11 kur. 15-31

Mazungumzo Ya Familia

Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?

Soma Esta 5:9–6:14. Ni mambo gani matatu katika picha hii ambayo si sahihi? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini, na ukamilishe picha hii kwa kuipaka rangi.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Kwa nini Hamani alimchukia Mordekai?

Dokezo: Soma Esta 5:9.

Kiburi kilimfanya Hamani afikie mkataa gani wenye makosa?

Dokezo: Soma Esta 6:6.

Ni nini kilichompata Hamani?

Dokezo: Soma Esta 7:9, 10.

Ni kwa njia gani unaweza kuepuka kuwa kama Hamani?

Dokezo: Soma Methali 16:18, 19; Yakobo 4:6.

UTENDAJI WA FAMILIA:

Someni simulizi hilo la Biblia pamoja. Ikiwezekana, mmoja asome sehemu ya msimuliaji, wa pili asome sehemu ya Hamani, wa tatu asome sehemu ya Zereshi na watumishi, na wanne asome sehemu ya mfalme.

Kusanya na Ujifunze

Kata, kunja katikati, na uhifadhi

KADI YA BIBLIA 4 ESTA

MASWALI

A. Esta aliwekwa malkia badala ya nani?

B. Kamilisha sentensi hii ya Biblia: “Esta alikuwa akizidi kupata . . .”

C. Jaza mapengo. Jina la Kiebrania la Esta lilikuwa ________, na binamu yake ________ mwenye umri mkubwa kuliko yeye akawa mlezi wake.

[Chati]

4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.

Adamu aumbwa Aliishi miaka Kitabu cha mwisho

ya 400 K.W.K. cha Biblia kinaandikwa

[Ramani]

Esta aliishi Shushani, jiji la Milki ya Muungano wa Umedi na Uajemi

UMEDI

Shushani

UAJEMI

ESTA

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Yatima ambaye alikuja kuwa malkia wa Mfalme Ahasuero Mwajemi. Esta alihatarisha maisha yake ili aripoti njama ya kuwaangamiza Wayahudi. (Esta 4:11, 15, 16) Sifa zake za ujasiri, busara, na roho yake ya kujitiisha zilikuwa muhimu zaidi kuliko urembo wake.—Esta 2:7; 1 Petro 3:1-5.

MAJIBU

A. Vashti.—Esta 1:12; 2:16, 17.

B. “. . . kibali machoni pa kila mtu aliyemwona.”—Esta 2:15.

C. Hadasa (linalotokana na Mhadasi), Mordekai—Esta 2:7.

Watu na Nchi

4. Jina langu ni You-Jin. Nina umri wa miaka 7 na ninaishi nchini Korea, barani Asia. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Korea? Ni 9,700, 37,900, au 96,600?

5. Ni nukta gani inayoonyesha eneo ninamoishi? Chora duara kuizunguka na utie nukta kuonyesha eneo unaloishi, kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Korea.

A

B

C

D

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

● Majibu ya ukurasa wa 30 na 31 kwenye ukurasa wa 15

MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31

1. Mordekai hapaswi kuwa amepanda gari, anapaswa kuwa amepanda farasi wa mfalme.

2. Mordekai anapaswa kuwa amevaa mavazi ya kifalme si mavazi ya kawaida.

3. Mordekai alipita kwenye kiwanja cha watu wote si nje ya kuta.

4. 96,600.

5. D.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki