Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/11 uku. 3
  • Kuteseka Kunapaswa Kwisha!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuteseka Kunapaswa Kwisha!
  • Amkeni!—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Watu Wanateseka Sana?
    Amkeni!—2011
  • Biblia Inasema Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Swali la 3: Kwa Nini Mungu Anaruhusu Niteseke?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Ikiwa Muumba Anajali, Mbona Wanadamu Wanateseka Sana?
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 7/11 uku. 3

Kuteseka Kunapaswa Kwisha!

Kuteseka kwa Khieu kulianza baba yake alipouawa kwa sababu ya kuacha ng’ombe wake waingie katika shamba fulani la mahindi. Baadaye, mama yake na dada zake wawili waliuawa na wanamgambo wa Khmer Rouge wa Kambodia. Kisha Khieu akajeruhiwa na bomu lililotegwa ardhini. Alikaa siku 16 msituni akisubiri msaada. Ilibidi mguu wake ukatwe. “Sikutaka kuendelea kuishi,” anasema Khieu.

HUENDA umeona kwamba kila mtu huteseka. Misiba ya asili, magonjwa, ulemavu, uhalifu wenye jeuri, na misiba mingine inaweza kumpata mtu yeyote, wakati wowote, mahali popote. Mashirika ya kutoa msaada yamejitahidi sana kuzuia au kupunguza kwa kiasi fulani kuteseka kwa wanadamu. Lakini jitihada zao zimetimiza nini?

Fikiria mfano mmoja—jitihada za kukabiliana na njaa. Kulingana na gazeti Toronto Star, misiba ya asili imewaacha watu wengi bila makao wala chakula. Hata hivyo, gazeti hilo linaripoti kwamba “jitihada za mashirika mengi za kupunguza njaa zinavurugwa na jeuri inayozidi kuongezeka.”

Viongozi wa kisiasa, kijamii, na kitiba wamefanya yote wanayoweza kupunguza kuteseka, lakini hawajafanikiwa. Programu za kuchochea ukuzi wa kiuchumi hazijakomesha umaskini. Chanjo, dawa, na maendeleo katika mbinu za kufanya upasuaji haziwezi kukomesha magonjwa yote. Maofisa wa polisi na vikosi vya kudumisha amani hawajui la kufanya kwa sababu ya kuongezeka kwa uhalifu wenye jeuri.

Kwa nini wanadamu wanateseka sana? Je, Mungu anajali wanadamu wanapoteseka? Kama tutakavyoona, mamilioni ya watu wamepata majibu yenye kufariji ya maswali hayo katika Biblia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki