Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/15 uku. 3
  • Je, Unaongoza Maisha Yako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Unaongoza Maisha Yako?
  • Amkeni!—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Changamoto: Kulemewa na Shughuli
    Amkeni!—2015
  • Changamoto: Hali Zisizoweza Kubadilika
    Amkeni!—2015
  • Kitu Ambacho Kinadumu Kuliko Sanaa
    Amkeni!—2007
  • Changamoto: Hisia Zisizofaa
    Amkeni!—2015
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2015
g 7/15 uku. 3
Mwanamume mwenye huzuni akiwaza kazini

HABARI KUU

Je, Unaongoza Maisha Yako?

ULIPOKUWA kijana, ulikuwa na malengo gani maishani? Huenda ulitaka kuoa au kuolewa, kujifunza stadi, au kupata kazi nzuri. Hata hivyo, mara nyingi mambo huwa tofauti na vile tulivyopanga. Changamoto zisizotarajiwa zinaweza kubadili kabisa malengo yetu. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Anja, Delina, na Gregory.

Anja, Delina, na Gregory
  • Anja, kutoka Ujerumani, aligunduliwa kuwa ana kansa alipokuwa na umri wa miaka 21, na kufikia sasa hawezi kutoka nyumbani.

  • Delina, kutoka Marekani, ana ugonjwa wa neva za misuli unaoitwa dystonia. Pia, anawatunza ndugu zake watatu wenye ulemavu.

  • Gregory, kutoka Kanada, ana ugonjwa wa kuwa na wasiwasi kupita kiasi.

Licha ya hali wanazokabili, Anja, Delina, na Gregory wameweza kuongoza maisha yao. Jinsi gani?

Methali moja katika Biblia inasema hivi: “Je, umejionyesha kuwa umevunjika moyo siku ya taabu? Nguvu zako zitakuwa chache.” (Methali 24:10) Matumizi yake ni wazi: Mtazamo unaweza kuathiri hali ya mtu. Watu wenye mtazamo usiofaa kujihusu wanapoteza uwezo wa kujiongoza, lakini wale wenye mtazamo unaofaa kujihusu mara nyingi wanapata nguvu ya kuwawezesha kuendelea kuongoza maisha yao.

Ona jinsi kufanya hivyo kulivyowasaidia Anja, Delina, na Gregory.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki