Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/15 uku. 7
  • Je, Unaweza Kuongoza Maisha Yako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Unaweza Kuongoza Maisha Yako?
  • Amkeni!—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Changamoto: Hali Zisizoweza Kubadilika
    Amkeni!—2015
  • Changamoto: Hisia Zisizofaa
    Amkeni!—2015
  • Maswali Ambayo Huenda Umejiuliza
    Amkeni!—2019
  • Je, Utakuwepo Katika Ulimwengu Mpya?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2015
g 7/15 uku. 7

HABARI KUU | JE, UNAONGOZA MAISHA YAKO?

Je, Unaweza Kuongoza Maisha Yako?

Mwanamume akiongoza boti yake

KUNA msemo usemao, “Maisha bila adha huwa malegevu.” Leo, hakuna mtu ambaye hajawahi kukabiliana na matatizo. Mara nyingi, siri ya mafanikio ni kujifunza kukubaliana na hali na kufanya mambo kulingana na hali hizo. Ni jambo linalofaa ikiwa utaweza kukabiliana vema na changamoto hizo maishani. Hatimaye, itakuwa vema ikiwa hali zako zitakuwa nzuri. Hata hivyo, jambo bora zaidi linakuja.

Biblia inaahidi wakati ambapo watu wote watakuwa na uwezo wa kuongoza maisha yao. Wataweza kuishi wakiwa na uwezo wa kutimiza mambo kikamili, bila kuwa na mahangaiko, mikazo ya kila siku, na hisia zisizofaa. (Isaya 65:21, 22) Biblia inaitaja hali hiyo kuwa “uzima ulio wa kweli.”—1 Timotheo 6:19.

“Na hakika wao watajenga nyumba na kukaa ndani yake; na hakika wao watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake. Hawatajenga na mtu mwingine akae ndani yake; hawatapanda na mtu mwingine ale. Kwa maana siku za watu wangu zitakuwa kama siku za mti; na watu wangu waliochaguliwa wataitumia kazi ya mikono yao wenyewe kikamilifu.”—Isaya 65:21, 22.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki