Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g20 Na. 2 kur. 8-9
  • Je, Tunapaswa Kujilaumu Tunapoteseka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Tunapaswa Kujilaumu Tunapoteseka?
  • Amkeni!—2020
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini ni Muhimu Kupata Jibu la Swali Hilo?
  • Jambo la Kufikiria
  • Mambo Ambayo Biblia Inafundisha
  • Biblia Inasema Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2020
  • Swali la 3: Kwa Nini Mungu Anaruhusu Niteseke?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Kwa Nini Watu Wanateseka Sana?
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2020
g20 Na. 2 kur. 8-9
Mwanamume amekaa sebuleni akiwa ameshika sigara kwenye mkono mmoja na mkono mwingine ameshika bia.

2. Je, Tunapaswa Kujilaumu Tunapoteseka?

Kwa Nini ni Muhimu Kupata Jibu la Swali Hilo?

Ikiwa jibu ni ndiyo, basi huenda tunaweza kupunguza matatizo tunayokabili.

Jambo la Kufikiria

Wanadamu wamechangia kwa kiasi gani kuwepo kwa matatizo yafuatayo?

  • Picha ya mkono uliokunja ngumi, ikiwakilisha jeuri.

    Kutendewa Vibaya.

    Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kwamba mtu mmoja kati ya watu wanne aliwahi kutendewa vibaya alipokuwa mtoto na mwanamke mmoja kati ya watatu hutendewa vibaya kimwili au kingono (au yote mawili) katika maisha yake.

  • Picha ya makaburi, ikiwakilisha vifo.

    Vifo.

    Takwimu ya Afya ya mwaka 2018 iliyochapishwa na Shirika la Afya Duniani inasema hivi; “Inakadiriwa kwamba watu 477,000 waliuawa duniani kote mwaka wa 2016.” Idadi hiyo inatia ndani watu 180,000 hivi ambao inawezekana waliuawa kwenye vita au vurugu zilizotokea mwaka huo.

  • Picha ya moyo, ikiwakilisha matatizo ya afya.

    Matatizo ya Afya.

    Makala iliyochapishwa kwenye jarida la National Geographic ya Fran Smith ilisema kwamba watu zaidi ya bilioni moja huvuta sigara na inasemekana kwamba sigara ni mojawapo ya chanzo cha magonjwa yanayosababisha vifo vya watu wengi kama vile magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa ya mapafu.

  • Picha ya mzani ulioegemea upande mmoja, ikionyesha hali kutokuwa na usawa katika jamii.

    Kutokuwa na Usawa Katika Jamii.

    Mwanasaikolojia Jay Watts anasema hivi: “Umaskini, kutokuwa na usawa katika jamii, kubaguliwa kwa sababu ya rangi, ubaguzi wa kijinsia, kulazimishwa kuhama eneo unaloishi au kuishi katika jamii yenye mashindano husababisha mkazo, kushuka moyo, mahangaiko na hofu.”

    JIFUNZE MENGI ZAIDI

    Tazama video Kwa Nini Mungu Aliiumba Dunia? kwenye jw.org/sw.

Mambo Ambayo Biblia Inafundisha

Mwanamume aliye kwenye picha iliyotangulia amelazwa hospitalini. Mke wake amehuzunika baada ya kupata habari mbaya kuhusu afya ya mume wake kutoka kwa daktari.

Matatizo mengi yaliyopo ulimwenguni leo yamesababishwa na wanadamu.

Matatizo mengi yamesababishwa na serikali zenye ukandamizaji zinazodai kuhangaikia masilahi ya raia wake na hivyo kufanya maisha yawe magumu kwa wanadamu.

“Mwanadamu amemtawala mwanadamu mwenzake kwa kumuumiza.”​—MHUBIRI 8:9.

Tunaweza kupunguza matatizo.

Kanuni za Biblia zinatutia moyo tuwe na afya nzuri na uhusiano mzuri pamoja na wengine.

“Moyo mtulivu huupa mwili uzima, lakini wivu huozesha mifupa.”​—METHALI 14:30.

“Acheni kabisa kila aina ya chuki yenye uhasama, hasira, ghadhabu, kufoka, matusi, na mambo yote yanayodhuru.”​—WAEFESO 4:31.

Je, tunapaswa kujilaumu tunapoteseka?

Biblia inasema hivi: “Lolote analopanda mtu, ndilo atakalovuna pia.” (Wagalatia 6:7) Huenda tukateseka kwa sababu ya mambo tunayochagua kufanya. Ndio sababu madaktari wanawashauri watu wale vyakula vyenye lishe, wafanye mazoezi na waepuke mazoea yenye kudhuru kama vile kuvuta sigara. Hata hivyo, haingefaa kusema kwamba matatizo yote yanasababishwa na wanadamu. Watu wengi wameathiriwa na aksidenti, majanga na matatizo mengine bila kutarajia.

Kwa nini watu wanaotenda mema wanateseka?

Utapata jibu kwenye swali la 3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki