Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 17 kur. 71-74
  • Watu Wawili Ambao Hawakusema Kweli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Watu Wawili Ambao Hawakusema Kweli
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Hatupaswi Kusema Uwongo?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Petro na Anania Walidanganya—Tunajifunza Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Semeni Ukweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
  • Kusema Uwongo—Je, Kwaweza Kutetewa Wakati Wowote?
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 17 kur. 71-74

Sura ya 17

Watu Wawili Ambao Hawakusema Kweli

TUSEME mtoto wa kike akimwahidi mama yake, “Ndiyo, nitarudi nyumbani mara ya kumaliza masomo.” Lakini ndipo watoto wengine wamwambie akae na kucheza nao. Ingekuwa vizuri kukaa kidogo tu?—

Au labda mtoto wa kiume amwahidi baba yake, “Hapana, sitatupia mpira tena nyumbani.” Je! ingekuwa vizuri kufanya mara chache tena wakati baba yoke hatazami?—

Mwalimu Mkuu alionyesha jambo zuri kufanya. Alisema hivi: ‘Neno lenu Ndiyo na limaanishe Ndiyo, na Siyo, Siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.’—Mathayo 5:37.

Kwa hayo Yesu alimaanisha nini?— Alimaanisha imetupasa sikuzote tutimize ahadi zetu; imetupasa sikuzote tuseme kweli.

Kuna hadithi inayoonyesha namna ilivyo maana kusema kweli. Ni juu ya watu wawili waliosema walikuwa wanafunzi wa Yesu.

Kitambo kidogo alipokwisha kufa Yesu, watu wengi wakawa wanafunzi wake. Wengine kati ya watu hawa walikuwa wamekuja Yerusalemu kutoka mbali. Kwa mara ya kwanza walijifunza hapa juu ya Yesu. Walitaka kujua zaidi. Kwa sababu hii wakakaa Yerusalemu kwa muda zaidi kuliko walivyotazamia. Wengine wao waka-pungukiwa fedha wakataka msaada waweze kununua chakula.

Wanafunzi katika Yerusalemu wakataka kuwasaidia. Basi, wengi wa wanafunzi hawa wakauza mali zao wakapeleka fedha kwa mitume wa Yesu. Ndipo mitume wakawapa fedha wale waliotaka.

Mwanafunzi jina lake Anania na mke wake Safira waliuza shamba lao. Hapana mtu aliyewaambia waliuze. Wenyewe waliamua. Lakini walilofanya halikuwa kwa sababu waliwapenda wanafunzi wapya. Kwa kweli, walitaka watu wafikiri walikuwa bora kuliko walivyokuwa kweli. Basi wakaamua kufanya ionekane kana kwamba walikuwa wakitoa fedha hizi zote kusaidia wengine. Lakini kwa kweli walitaka kutoa nusu yake tu na kuchukua zinazobaki. Wewe waonaje juu ya hilo?—

Basi, Anania akaja kuwaona mitume wa Yesu kwanza. Akawapa fedha. Lakini Anania hakuwa akitoa fedha zote. Mungu alijua hili. Basi akamjulisha mtume Petro kwamba Anania hakuwa akisema kweli. Ndipo Petro akasema:

‘Anania, mbona umemwacha Shetani akufanye utende hivi? Shamba lilikuwa lako. Haikuwa lazima uliuze. Na hata ulipokwisha kuuza shamba, ilikuwa juu yako kuamua ungefanyaje na fedha. Lakini kwa nini ulisingizia kutoa fedha zote hali ulijua ulikuwa ukitoa nusu yake tu? Kwa hili ulikuwa ukisema uongo, si kwetu tu, bali kwa Mungu.

Lilikuwa jambo zito sana. Anania alikuwa akisema uongo! Hakufanya jambo ambalo ali-sema angefanya. Yeye na mke wake walisingizia tu kufanya.

Biblia inatuambia lililofuata kutukia. Inasema hivi: ‘Aliposikia maneno ya Petro, Anania akaanguka akafa.’ Mungu alimpiga Anania akafa! Mwili wake ulitolewa nje ukazikwa.

Yapata kama saa tatu hivi tokea hapo Safira mke wake akaingia. Hakuwa na habari ya jambo lililompata mume wake. Basi Petro akamwuliza: ‘Je! ninyi wawili mliuza shamba kwa kadiri ya fedha mliyotupa?

Safira akajibu: ‘Ndiyo, tuliuza shamba kwa kadiri hiyo tu.’

Lakini huo ulikuwa uongo! Walikuwa wamechukua sehemu ya fedha wenyewe. Basi Mungu akampiga Safira akafa naye.—Matendo 5:1-11.

Unafikiri kuna jambo ambalo imetupasa tujifunze kutokana na yaliyowapata Anania na Safira?— Ndiyo. Inatufundisha kwamba Mungu hapendi waongo. Anataka sikuzote tuseme kweli.

Watu wengi wanasema si vibaya kusema uongo. Karibu kila siku wanasema uongo. Lakini unafikiri ni vizuri?—

Ulijua kwamba magonjwa yote, maumivu na mauti vilivyopo duniani vilitokea kwa sababu ya uongo?— lbilisi alisema uongo kwa mwanamke wa kwanza Hawa juu ya Mungu. Mato-keo yake, akavunja sheria ya Mungu. Halafu akamshawishi Adamu naye avunje sheria ya Mungu. Sasa walikuwa watenda dhambi, nao watoto wao wote wangezaliwa watenda dhambi. Na kwa sababu ya dhambi wangepata taabu na kufa. Yote yalianzaje?— Na uongo.

Si ajabu Yesu alisema Ibilisi “ni mwongo, na baba wa [uongo].” Ndiye wa kwanza kusema uongo. Mtu ye yote asemapo uongo, anafanya aliyofanya Ibilisi. Imetupasa tufikirie hili wakati wo wote tunapoona tunashawishwa tuseme uongo.—Yohana 8:44.

Ni mara nyingi wakati mtu anapofanya kosa ndipo huenda akaona kushawishwa kusema uongo juu yake. Kwa mfano, huenda ukavunja kitu fulani. Pengine hukukusudia kufanya, hata hivyo kitu kikavunjika. Imekupasa ufanyeje?— Je! ujaribu kuficha na kutumaini hapana atakayejua?—

Imetupasa tukumbuke Anania na Safira. Walijaribu kuficha kweli. Naye Mungu alionyesha ubaya wa hilo kwa kuwapiga wakafa.

Basi, si kitu tufanye nini, tusiseme uongo juu yake hata kidogo. Biblia inasema: “Mkaseme kweli.” Tena inasema: “Msiambiane uongo.” Sikuzote Yehova anasema kweli, naye atutazamia tufanye vivyo hivyo.—Waefeso 4:25; Wakolosai 3:9.

(Imetupasa sikuzote tuseme kweli. Ndiyo maana itolewayo katika Kutoka 20:16; Mithali 6:16-19; 14:5; 12:19; 16:6.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki