Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 22 kur. 91-94
  • Mtu Aliyemsahau Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtu Aliyemsahau Mungu
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Ambacho Kwa Kweli Ni Cha Maana Maishani?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Je, Wewe Ni “Tajiri Kwa Mungu”?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Je, Ni Lazima Wakristo Wawe Maskini?
    Amkeni!—2003
  • Baraka ya Yehova Inatajirisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 22 kur. 91-94

Sura ya 22

Mtu Aliyemsahau Mungu

PALIKUWA na mtu aliyekuja kumwona Yesu siku moja. Alijua Yesu alikuwa mwenye hekima sana. Akamwambia Yesu: ‘Mwalimu, mwambie ndugu yangu anipe sehemu ya vitu alivyo navyo.’ Yule mtu alifikiri alikuwa na haki ya sehemu ya vitu hivyo.

Ikiwa ungalikuwa Yesu, ungalisemaje?— Yesu aliona mtu yule alikuwa na ugumu. Lakini ugumu haukuwa kwamba alitaka vitu ambavyo ndugu yake alikuwa navyo. Ugumu wa mtu yule ulikuwa kwamba hakujua lililokuwa la maana kweli katika maisha.

Basi Yesu akamwambia hadithi. Ilikuwa juu ya mtu aliyemsahau Mungu. Ungependa uisikie?—

Mtu fulani alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mashamba na ghala. Mazao aliyopanda yalizaa sana. Hakuwa na nafasi katika ghala zake kuweka mazao yate. Angefanyaje?

Yule tajiri akajisemesha mwenyewe: ‘Nitabomoa ghala zangu na kujenga zilizo kubwa zaidi. Ndipo nitaweka mazao yangu na vitu vyangu vyote vizuri katika ghala hizi mpya.’

Yule tajiri alifikiri hili lilikuwa jambo la hekima kufanya. Alifikiri alikuwa na akili sana kuweka akiba ya vitu vingi. Akajisemesha mwenyewe: ‘Nina vitu vizuri vingi vimewekwa akiba. Vitanichukua miaka mingi. Basi sasa naweza kustarehe. Nitakula, nitakunywa nijifurahishe mwenyewe.’

Lakini kulikuwako kosa fulani katika kufikiri kwa tajiri. Lilikuwa nini?— Alikuwa akifikiria yake mwenyewe tu na raha yake mwenyewe. Lakini alimsahau Mungu.

Basi Mungu akasema na tajiri. Akamwambia hivi: ‘Mtu mpumbavu wewe. Utakufa usiku wa leo. Basi nani atakuwa na vitu ulivyoweka akiba?’

Je! tajiri huyo angeweza kutumia vitu hivyo akiisha kufa?— Hapana; mwingine angevichukua. Yesu akasema: “Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”—Luka 12:13-21.

Hutaki uwe kama tajiri yule, sivyo?— Kusudi lake kuu katika maisha lilikuwa kupata mambo ya kimwili. Hilo lilikuwa ndilo kosa lake. Sikuzote alitaka zaidi.

Watu wengi wako kama tajiri yule. Sikuzote wanataka zaidi. Lakini hii inaweza kuongoza kwenye magumu makubwa.

Kwa mfano, unavyo vitu vya kuchezea, sivyo?— Ni nini kati ya vitu vya kuchezea ulivyo navyo? Niambie.—

Namna gani je! ikiwa mmoja wa rafiki zako ana motokaa ya mfano, au kitoto cha bandia au kitu fulani kingine cha kuchezea usichokuwa nacho? Je! ingefaa ujaribu kumnyang’anya?—

Huenda zikawako nyakati kitu cha kuchezea kinapoonekana cha maana sana. Lakini kinakuwaje wakati kunapita kitambo?— Kinachakaa. Pengine kinaharibika, ndipo hata hatukitaki te-na. Kwa kweli, unacho kitu bora zaidi sana kuliko vitu vya kuchezea. Unajua ni kitu gani?— Ni uhai wako. Na uhai wako wategemea kufanya yanayompendeza Mungu, sivyo?— Basi usiwe kama tajiri yule mpumbavu.

Si watoto tu wafanyao mambo kama tajiri huyo. Watu wazima wengi vile vile wanafanya. Wengine kati yao sikuzote wanataka zaidi ya vitu walivyo navyo. Huenda wakawa na chakula cha siku hiyo, nguo za kuvaa na nyumba. Lakini wanataka zaidi. Wanataka nguo nyingi sana. Na wanataka nyumba kubwa zaidi. Vitu hivi vinagharimu fedha. Hivyo wanafanya kazi sana ili wapate fedha nyingi. Na kadiri wapatavyo fedha zaidi, ndivyo wanavyotaka zaidi.

Watu wazima wengine wanashughulika sana wakijaribu kupata fedha hata wanakosa wakati wa kuwa pamoja na jamaa zao. Na hawana wakati wa mambo ya Mungu. Je! fedha zao zaweza kuwafanya waendelee kuishi? Hapana; Mungu peke yake aweza kufanya hivyo. Je! wanaweza kutumia fedha zao wakiisha kufa?— Hapa-na; kwa sababu waliokufa hawawezi kufanya lo lote hata kidogo.

Je! hiyo ina maana ni kosa kuwa na fedha?— Hapana. Kwa fedha twaweza kununua chakula. Kwa fedha tunanunua nguo. Biblia inasema kuwa na fedha ni ulinzi. Lakini ‘tukipenda’ fedha, basi tutapata taabu. Tutakuwa kama tajiri yule mpumbavu aliyejiwekea hazina asiwe tajiri kwa Mungu.—Mhubiri 7:12.

Mwalimu Mkuu alisema kwamba tajiri yule alikuwa mpumbavu kwa sababu ‘hakujitajirisha kwa Mungu.’ Maana yake nini ‘kujitajirisha kwa Mungu’?— Maana yake ni kumweka Mungu kwanza katika maisha zetu. Watu wengine wanasema kwamba wanamwamini Mungu. Huenda hata wanasoma Biblia mara kwa mara. Na wanafikiri ni basi. Lakini je! ‘wanajitajirisha’ kweli kwa Mungu?—

Mtu aliye tajiri ana zaidi kuliko kidogo. Ana mengi. Ikiwa ‘anajitajirisha kwa Mungu,’ maisha yake yanajaa mawazo mengi juu ya Mungu. Anajifurahisha kusema juu ya Mungu mara nyingi. Sikuzote anafanya ambayo Mungu anamwambia kufanya. Na anatumia wakati wake pamoja na watu wampendao Mungu.

Je! sisi ni watu wa namna hiyo? Je! ‘tunajitajirisha kwa Mungu’?— Tukijifunza kweli kweli kwa Mwalimu Mkuu, tutakuwa hivyo.

(Hapa pana maandiko zaidi yanayoonyesha maoni yanayofaa kuwa nayo kwa mambo ya kimwili: 1 Timotheo 6:6-10; Mithali 23:4; 28:20; Waebrania 13:5.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki