Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 33 kur. 135-138
  • “Vya Kaisari Mpeni Kaisari”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Vya Kaisari Mpeni Kaisari”
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi ya Kujua Yule Tunayepaswa Kumtii
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Je, Unapaswa Kulipa Kodi?
    Amkeni!—2003
  • Je, Uko “Tayari Kutii”?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Je, Ni Lazima Ulipe Kodi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 33 kur. 135-138

Sura ya 33

“Vya Kaisari Mpeni Kaisari”

NA TUCHUKUE fedha tuitazame. Unaona nini juu ya fedha? — Nani alitengeneza fedha hii?— Ni serikali. Kwa maelfu ya miaka serikali zimetengeneza fedha ambazo watu wanatumia. Wakati Mwalimu Mkuu alipokuwa duniani, serikali ya Kirumi ilitengeneza fedha. Unamjua aliyekuwa mtawala wa serikali hiyo?— Aliitwa Kaisari.

Serikali ya Kirumi ilifanyia watu mambo mengi mazuri katika siku hizo. Na serikali leo zinatufanyia sisi mambo mengi mazuri. Zinatengeneza barabara za kutembea. Zinawalipa mishahara mapolisi na wazima moto ili kutulinda sisi.

Inagharimu serikali fedha kufanya mambo haya. Unajua serikali inapata wapi fedha?— lnapata kwa watu. Fedha ambayo watu wanalipa kwa serikali inaitwa kodi.

Watu wengi hawapendi kulipa kodi. Yesu alipokuwa duniani, wengine kati ya Wayahudi hawakutaka kulipa kodi zo zote kwa serikali ya Kirumi. Walichukia kodi hizo. Basi, siku moja watu fulani wakamjia Mwalimu Mkuu wakamwuliza hivi: ‘Je! ni lazima tulipe kodi kwa Kaisari au sivyo?’

Sasa, wale watu waliuliza ulizo hili ili kumtega Yesu. Kwa maana ikiwa Yesu angejibu, ‘Ndiyo, ni lazima mlipe kodi,’ Wayahudi wengi wasingependa ambayo Yesu angesema. Lakini Yesu asingeweza kusema, ‘Hapana, si lazima mlipe kodi.’ Ingekuwa kosa kusema hivyo.

Basi hivi ndivyo Yesu alivyofanya. Aliwaambia wale watu: ‘Nionyesheni fedha.’ Walipomletea fedha, Yesu akawauliza: ‘Ni ya nani picha na jina juu yake?’

Wale watu wakasema: “Ya Kaisari.” Basi Yesu akasema: “Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu.”—Luka 20:19-26.

Je! hilo halikuwa jibu zuri?— Hakuna mtu ambaye angeweza kuona kosa lo lote kwa hilo. Ikiwa Kaisari anawafanyia watu mambo, ni haki kabisa kutumia fedha ambayo Kaisari alitengeneza kumlipa kwa mambo haya. Hivyo katika njia hii Yesu alionyesha kwamba ni haki kulipa kodi kwa serikali kwa mambo ambayo tunapokea.

Sasa, huenda usiwe mwenye umri wa kulipa kodi. Lakini kuna jambo fulani ambalo imekupasa kuipa serikali. Unajua hilo ni nini?— Ni kutii sheria za serikali.

Ni Mungu anayetuambia hili. Neno lake linasema hivi: ‘Mwitii mamlaka iliyo kuu.’ Na ‘mamlaka iliyo kuu’ ni nini?— Ni wale watu wenye uwezo katika serikali. Basi kweli imetupasa tutii sheria. Mungu anasema hivyo.—Warumi 13:1, 2.

Angalia mfano. Huenda kukawa sheria inayokataza kutupa karatasi au takataka nyingine barabarani. Je! imekupasa utii sheria hiyo?— Ndiyo, Mungu anataka uitii.

Je! imetupasa tutii mapolisi vile vile? — Serikali inawalipa mishahara mapolisi walinde watu. Kuwatii wao ni kama kuitii serikali.

Basi ikiwa unataka kuvuka barabara na polisi anasema, “Ngoja!” imekupasa ufanyeje?— Namna gani je! wengine wakivuka, maana yake imekupasa uvuke?— Hata ikiwa ni wewe peke yako unangoja, ngoja. Mungu anatuambia tutii.

Pengine kuna matata katika ujirani naye polisi asema, “Usipite barabarani. Usitoke nje.” Lakini huenda utasikia kelele na kutaka kujua kuna nini. Je! utoke ukaone?— Je! huku kungekuwa kuitii ‘mamlaka iliyo kuu’?—

Mahali pengi serikali vile vile inajenga shule. Na inawalipa mishahara waalimu. Wakati watoto wanapofanya anayowaambia mwalimu, inaleta amani darasani. Basi unafikiri Mungu anataka umtii mwalimu?—

Hakuna andiko katika Biblia lisemalo, “Umtii mwalimu wako.” Lakini Biblia inaonyesha kwamba imekupasa kutii. Serikali inamlipa mwalimu mshahara ili afundishe, sawa kama inavyomlipa polisi alinde watu. Basi kumtii ama polisi ama mwalimu ni sawa na kutii serikali.

Au twaweza kulitazama katika njia hii. Mungu anawaambia watoto ‘kumtii ba-ba na mama yao.’ Lakini baba na mama yako wamekupeleka shuleni kwa mwalimu akuangalie. Basi ni vizuri kumtii mwalimu wako, kama unavyowatii wazazi wako nyumbani.—Waefeso 6:1.

Mimi siko pamoja nawe sikuzote. Hivyo huenda nisione kwamba wamtii mwalimu. Lakini Mungu anaona. Na ni Mungu ambaye kweli tunataka tumpendeze, sivyo?— Tena, huenda nisione ikiwa unamtii polisi. Lakini nani anayeona?— Ni Mungu. Kumbuka hilo sikuzote.

Kumbuka, tena, kwamba Mungu ndiye wa kwanza katika maisha zetu. Tunaitii serikali kwa sababu ndivyo Mungu anataka tufanye. Lakini namna gani wakituambia kufanya ambalo Mungu anasema tusifanye? Ikiwa ye yote anatuambia, “Si lazima kumtii Mungu,” je! Mungu anataka tusikilize hilo?—

Hilo lilitukia kwa mitume wa Yesu. Sasa mitume wangefanyaje? Wewe ungalifanyaje?— Walijibu hivi: “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.”—Matendo 5:29.

(Kuheshimu sheria kunafundishwa katika Biblia. Soma yaliyoandikwa katika Tito 3:1, Mathayo 5:41 na 1 Petro 2:12-14.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki