Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 37 kur. 151-154
  • Mtume Aliyegeuka Akawa Mwivi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtume Aliyegeuka Akawa Mwivi
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Usiwe Mwizi Kamwe!
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • “Injili ya Yuda” Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Kristo Asalitiwa na Kukamatwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 37 kur. 151-154

Sura ya 37

Mtume Aliyegeuka Akawa Mwivi

JE! MTU ye yote amepata kuiba cho chote kutoka kwako?— Uliona namna gani juu yake? Ye yote aliyeiba alikuwa mwivi, na hakuna mtu anayependa mwivi.

Je! ulijua kwamba mmoja wa mitume wa Yesu aligeuka akawa mwivi? Jina lake alikuwa Yuda Iskariote.

Yuda alijua mambo ambayo ilikuwa vizuri kufanya. Hata wakati alipokuwa mtoto mdogo alikuwa amesikia sheria ya Mungu. Alijua kwamba wakati mmoja Mungu alikuwa hata amesema kutoka mbinguni kwa sauti kuu akawaambia watu wake: “Usiibe.” Yuda alijua kwamba sheria ya Mungu ilikuwa kweli.—Kutoka 20:15.

Wakati alipokuwa mtu mzima alikutana na Mwalimu Mkuu. Yuda alipenda mambo ambayo Yesu alisema. Yuda akawa mwanafunzi wa Yesu. Wakati ulipofika, Yesu hata alimchagua Yuda awe mmoja wa mitume wake kumi na wawili.

Yeye na mitume wake walitumia wakati mwingi wakiwa pamoja. Walisafiri pamoja. Walikula pamoja. Na fedha za kikundi ziliwekwa pamoja katika kisanduku. Yesu alimpa Yuda kisanduku hicho akitunze.

Kwa kweli, fedha hazikuwa mali ya Yuda. Yesu ndiye angemwambia namna ya kuzitumia. Lakini unajua Yuda alifanya nini punde kidogo? Yeye alianza kuchukua fedha katika kisanduku wakati hakuambiwa afanye hivyo. Yeye alichukua wakati wengine walipokuwa hawatazami. Aligeuka akawa mwivi. Sasa alianza kufikiri juu ya fedha wakati wote. Alijaribu kutafuta njia za kupatia fedha zaidi.

Siku moja mwanamke alichukua mafuta mazuri sana naye akayatumia juu ya miguu ya Yesu ili kumburudisha. Lakini Yuda alinung’unika. Alisema kwamba mafuta yamepaswa yauzwe ili wawe na fedha zaidi za kuwapa maskini. Kwa kweli yeye alitaka kuweka fedha zaidi katika kisanduku ili aweze kuiba. Wewe unafikiri namna gani juu ya mtu kama huyo?— —Yohana 12:1-6.

Wakati huo Yesu hakumwambia Yuda kwamba alikuwa mwivi. Lakini alimwambia asimsumbue mwanamke ambaye alikuwa amekuwa mwema sana. Yuda hakupenda hilo. Angefanya nini?

Ingalimfaa asikitike. Ingalimfaa amwambie Yesu kwamba alikuwa amekuwa akiiba, na ingalimfaa arudishe zile fedha. Lakini, kuliko kufanya hivyo, yeye alifanya jambo baya sana.

Alikwenda kwa makuhani wakuu, waliokuwa adui za Yesu. Walitaka kumkamata Yesu. Lakini walitaka wafanye hivyo usiku ili watu wasiwaone. Yuda aliwaambia: ‘Mimi nitawaambia ninyi namna mnavyoweza kumkamata Yesu, ikiwa mtanipa fedha. Mtanipa ngapi?’ Makuhani walisema: ‘Sisi tutakupa vipande 30 vya fedha!’ Hizo zilikuwa fedha nyingi.—Mathayo 26:14-16.

Yuda mbaya sana akachukua fedha. Ilikuwa kana kwamba alikuwa akimwuza Mwalimu Mkuu kwa watu hao. Unaweza kuwazia mtu ye yote akifanya jambo baya sana kama hilo?— Basi, hivyo ndivyo inavyokuwa wakati mtu anapokuwa mwivi. Yeye anapenda fedha zaidi kuliko anavyompenda Mungu.

Sasa, na tuhakikishe kwamba tunafahamu vizuri jambo hili. Kufahamu namna mwivi alivyo, ni lazima tujue maana yake nini kuwa na kitu fulani. Watu wanakuwa na vitu kwa sababu walivifanyia kazi. Au walivinunua kwa fedha. Au labda walipewa kama zawadi.

Wakati baba yako anapofanya kazi analipwa fedha kwa kazi hiyo. Je! fedha hizo zinakuwa zake?— Ndiyo, kwa sababu alizifanyia kazi. Si zako wewe; ni zake yeye.

Kwa fedha hizo yeye ananunua vitu vya nyumbani mwenu. Hivyo ni vitu vyake. Kwa sababu ni vitu vyake, yeye ana haki kusema nani anaweza kuvitumia. Anakuambia ikiwa unaweza kuvichezea au sivyo. Na labda anamwacha mama yako akuambie tena juu ya hili.

Mara nyingine unakwenda kucheza na watoto wengine katika nyumba yao, sivyo?— Vitu vilivyo katika nyumba yao ni vya baba yao. Je! ingekuwa vizuri kuchukua kitu fulani kutoka katika nyumba yao na kukipeleka nyumbani kwenu?— Sivyo, isipokuwa baba au mama yao anakuambia uchukue. Ikiwa unakwenda na kitu fulani nyumbani kwenu bila kuwaomba, huo ungekuwa wivi.

Sababu gani mtu anaiba?— Labda anaona kitu fulani ambacho ni cha mtu mwingine. Labda ni baisikeli. Kwa kadiri anavyoitazama baisikeli hiyo na kufikiri juu yake, ndivyo anavyoipenda zaidi. Ikiwa yeye si mtu mwenye upendo, hajali namna mtu mwingine anavyoona. Hivyo pengine atampiga mtu mwingine na kujaribu kuchukua baisikeli kutoka kwake. Au labda atangojea mpaka wakati ambao mtu mwingine hatazami. Ndipo anachukua baisikeli. Yeye anafanya nini kweli? Anaiba.

Labda mtu mwingine haoni wakati anapoiba baisikeli. Lakini mtu fulani anamwona akiiba. Unajua ni nani huyo?— Yehova Mungu anamwona akiiba. Mungu anaona kwamba yeye ni mwivi.

Haifanyi tofauti yo yote ikiwa mtu mwingine ana vitu vingi au vichache tu. Watu wengine wanakwenda dukani na kuona vitu vingi kule. Wanaona kitu fulani ambacho wanataka sana sana. Pengine watajiambia wenyewe kwamba hakuna mtu atakayejua kama kunakosekana kitu kimoja. Basi wanakichukua, lakini hawalipi kwa kitu hicho. Je! hivyo ni vizuri?— Sivyo, ni wivi.

Wakati watu wanapofanya hivyo, wanafanana na Yuda. Kwa sababu Yuda alikuwa mwivi! Na tuhakikishe tusije tukawa kama yeye.

(Ni makosa kuiba. Biblia inaonyesha kwa wazi katika Marko 10:17-19; Warumi 13:9; Waefeso 4:28.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki