Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 66
  • Yezebeli—Malkia Mbaya Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yezebeli—Malkia Mbaya Sana
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Malkia Mwovu Aadhibiwa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Sasa Ndio Wakati wa Kuchukua Hatua
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Alivumilia Licha ya Ukosefu wa Haki
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • “Nyumba Yote ya Ahabu Itaangamia”—2Fa 9:8
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 66
Wanaume wa jumba la mfalme wakiwa tayari kumtupa Malkia Yezebeli kupitia dirishani

HADITHI YA 66

Yezebeli—Malkia Mbaya Sana

BAADA ya Mfalme Yeroboamu kufa, kila mfalme anayetawala ufalme wa kaskazini wa makabila 10 ya Israeli ni mbaya. Mfalme Ahabu ndiye mfalme mbaya sana kuliko wote. Unajua sababu? Sababu moja kubwa ni mke wake, Malkia mbaya sana Yezebeli.

Yezebeli si mwanamke Mwisraeli. Ni binti ya mfalme wa Sidoni. Yezebeli anachukia Yehova tena anaua manabii wake wengi. Yezebeli akitaka kitu, anamwua mtu ili akipate.

Siku moja Mfalme Ahabu anahuzunika sana. Basi Yezebeli

anamwuliza hivi: ‘Kwa nini una huzuni leo?’

‘Kwa sababu ya maneno ya Nabothi,’ Ahabu anajibu. ‘Nilitaka kununua shamba lake la mizabibu. Lakini akakataa.’

‘Usihangaike,’ Yezebeli asema. ‘Nitakupatia.’

Basi Yezebeli anaandikia wakuu barua katika mji alimokuwa

akikaa mtu huyo Nabothi. ‘Waambieni watu wa ovyo-ovyo waseme kwamba Nabothi amemtukana Mungu na mfalme,’ anawaambia hivyo. ‘Kisha mmtoe Nabothi nje ya mji na kumpiga kwa mawe afe. ‘

Mara Yezebeli anapojua kwamba Nabothi amekufa, anamwambia Ahabu hivi: ‘Sasa nenda kachukue shamba lake.’ Yezebeli anapaswa kuadhibiwa kwa kufanya ubaya huo, sivyo?

Basi, wakati fulani, Yehova anamtuma Yehu akamwadhibu. Yezebeli anaposikia kwamba Yehu anakuja, anapaka macho yake rangi na kujipamba ili aonekane mrembo. Lakini Yehu anapokuja na kumwona Yezebeli katika dirisha, anawapazia sauti wanaume walio katika jumba la kifalme: ‘Mwangusheni chini!’ Wanaume hao wanatii, kama unavyowaona katika picha. Wanamwangusha chini, naye anakufa. Huo ndio mwisho wa Yezebeli Malkia mbaya sana.

1 Wafalme 16:29-33; 18:1-4; 21:1-16; 2 Wafalme 9:30-37.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki