Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 70
  • Yona na Samaki Mkubwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yona na Samaki Mkubwa
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Yehova Alimwonyesha Yona Subira
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Alijifunza Kutokana na Makosa Yake
    Igeni Imani Yao
  • Alijifunza Kutokana na Makosa Yake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Yona Ajifunza Juu ya Rehema ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 70
Kisa cha Yona kumezwa na samaki mkubwa

HADITHI YA 70

Yona na Samaki Mkubwa

TAZAMA mwanamume ndani ya maji. Ana taabu nyingi, sivyo? Samaki yuko karibu kummeza! Unamjua mtu huyu? Ni Yona. Na tuone alivyoingia katika taabu nyingi.

Yona ni nabii wa Yehova. Muda mfupi baada ya kufa nabii Elisha, Yehova amwambia Yona hivi: ‘Nenda kwenye mji wa Ninawi. Ubaya wa watu ni mkubwa sana, nataka ukawaambie hivyo.’

Lakini Yona hataki kwenda. Basi anapanda meli ambayo haiendi Ninawi. Yehova hafurahi kwa sababu Yona anakimbia. Basi anatokeza upepo mkubwa. Upepo huo karibu kuzamisha meli. Wasafiri wa meli wanaogopa sana na kuililia miungu yao iwasaidie.

baharia akitazama ubavuni mwa mashua  wakati Yona ametupwa ndani ya bahari

Mwishowe Yona anawaambia hivi: ‘Ninamwabudu Yehova, Mungu aliyeifanya mbingu na dunia. Ninakimbia kazi ya Yehova.’ Basi wasafiri wanamwuliza hivi: ‘Tukufanyie nini ili upepo utulie?’

‘Nitupeni baharini, na bahari itatulia,’ Yona asema. Wasafiri hao hawataki kufanya hivyo, lakini upepo unapozidi kuwa mbaya, wanamtupa Yona baharini. Mara upepo unatulia, na bahari inakuwa kimya tena.

Wakati Yona anapozama majini, samaki mkubwa anammeza. Lakini hafi. Anakuwa ndani ya tumbo la samaki huyo siku tatu mchana na usiku. Yona anasikitika sana kwa vile hakumtii Yehova aende Ninawi. Unajua analofanya sasa?

Yona anamwomba Yehova amsaidie. Ndipo Yehova anamwagiza samaki huyo amtapike Yona pwani. Baada ya hayo Yona aenda Ninawi. Je! hilo halitufundishi kutimiza agizo la Yehova?

Kitabu cha Biblia cha Yona.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki