Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 72
  • Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Mfalme Apata Thawabu kwa Sababu ya Imani Yake
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
  • Ametupa Uhuru wa Kuchagua
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Mfano wa Kuigwa—Hezekia
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Wachungaji Saba Na Watawala Wadogo Wanane Wanatuhusuje Leo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 72
Mfalme Hezekia anasali huku barua kutoka kwa mfalme wa Ashuru zikiwa zimetandazwa mbele ya madhabahu ya Yehova

HADITHI YA 72

Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia

UNAJUA sababu mwanamume huyu anamwomba Yehova? Kwa nini ameweka barua hizi mbele ya madhabahu ya Yehova? Mwanamume huyu ni Hezekia. Ni mfalme wa makabila mawili ya kusini ya Israeli. Ana taabu nyingi. Kwa nini?

Kwa sababu majeshi ya Ashuru yamekwisha haribu makabila 10 ya kaskazini. Yehova aliruhusu hayo yatokee kwa sababu watu hao walikuwa wabaya sana. Na sasa majeshi ya Ashuru yamekuja kupigana na ufalme wa makabila mawili.

Mfalme wa Ashuru amempelekea Mfalme Hezekia barua sasa hivi. Hizo ndizo barua ambazo Hezekia ameweka mbele za Mungu. Ni barua za kumcheka Yehova, na kumwambia Hezekia akubali kushindwa. Ndiyo sababu Hezekia anaomba hivi: ‘Ee Yehova, utuokoe na mfalme wa Ashuru. Ndipo mataifa yote yatakapojua wewe peke yako ndiwe Mungu.’ Yehova atamsikiliza Hezekia?

Hezekia ni mfalme mzuri. Yeye si kama wafalme wale wabaya wa ufalme wa Israeli wa makabila 10, wala si kama baba yake Ahazi, mfalme mbaya. Hezekia ametii sana sheria zote za Yehova. Basi, Hezekia akiisha kusali, nabii Isaya anampelekea ujumbe huu wa Yehova: ‘Mfalme wa Ashuru hataingia Yerusalemu. Askari zake hawataukaribia. Hawataupiga mji huo hata mshale mmoja.’

Miili ya wanajeshi wa Ashuru waliokufa

Itazame picha ya ukurasa huu. Unajua ni askari gani hawa wote waliokufa? Ni Waashuru. Yehova alimtuma malaika wake, na usiku mmoja malaika huyo akaua askari wa Ashuru 185,000. Lakini baada ya Hezekia kufa Manase mwanawe anakuwa mfalme. Manase na Amoni mwanawe anayemfuata ni wafalme wabaya sana. Hivyo nchi tena yajaa uhalifu na jeuri. Mfalme Amoni anapouawa na watumishi wake, Yosia mwanawe anafanywa mfalme wa ufalme wa makabila mawili.

2 Wafalme 18:1-36; 19:1-37; 21:1-25.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki