Wimbo 81
Shukrani kwa Ajili ya Subira ya Kimungu
1. Yehova u mwenye nguvu
Ulifanya vyote vyema.
Vyakushuhudia vyote,
Duniani, anga, kote.
Nao wajapovipenda
Wale kweli wanapenda,
Mengine watayaona
Ishindapo enzi yako.
2. Kwa adili ungeweza
Kukomesha mara ovu;
Bali tupate wokovu,
Hukutuangamiza, la.
Wale wenye jina lako
Washukuru subira’ko
Wakitamani kuona
Ushindi wa enzi yako.
3. Subira hatutapuza.
Habari tutahubiri,
Tuonyeshe watu sifa,
Zionyeshwazo na Neno.
Fanya njia iwe wazi
Wapate wokovu pia,
Kisha tuone uzuri
Ishindapo enzi yako.