Wimbo 90
Kumwabudu Yehova, Bwana Mwenye Enzi Kuu
1. Bwana Mwenye Enzi Kuu
Umerudisha ukweli.
Nuru yako yaja chini,
Na mamilioni waja.
2. Ni saa ya ongezeko
Kwao wahudumu wako.
Wanakuheshimu wewe
Wakuabudu pekee.
3. Na hawajifunzi vita,
Watanguliza huduma.
Wakuinamia wewe
Washika sheria zako.
4. Hii ni siku ya shangwe,
Ufalme ni wa kudumu!
Mwanao anatawala;
Tunashangilia hilo.