Wimbo 103
Mtupie Yehova Mzigo Wako
1. Bwana, sala usikie,
Usijifiche kwangu.
Sikiliza, unijibu,
Ili nisisumbuke.
(Korasi)
2. Kama ningekuwa njiwa
Ningeruka mbali na
Waovu, niwe salama,
Ndimi zao zigawe.
(Korasi)
3. Nitamuomba Yehova,
Anayeketi juu.
Japo kupingwa, amani
Hupa, atakomboa.
(KORASI)
Mutupie Yah muzigo;
Atakusaidia.
Hataacha utikiswe
Atakupa imara.