Wimbo 178
“Amani ya Mungu” Ipitayo Yote
1. Amani ya Mungu
Sana yote yapita
Yaondoa wasiwasi,
Na tuna utulivu
Yalinda akili
Yavuta moyo kwake
Daima tuko tayari
—Upande wa Ufalme.
2. Na mahangaiko
Watu wanaonea.
Fujo zinazidi nazo,
Zakera watu sana.
Hatukasiriki,
Mungu hatasahau.
Upendo, ulinzi wake
Unatupa amani.
3. Twatumai Mungu.
Atatimiza haja.
Anazo neema sana,
Na atatuongoza.
Na amani yake,
Yaleta shangwe nyingi.
Tufanyapo penzi lake,
’Tabarikiwa naye.