Wimbo 223
Washikamanifu Wako Watakubariki
1. Washikamanifu wako
Watakubariki,
Wakutangaze Yehova
Na kukutukuza.
Uko juu sana,
Unastahili sifa
Mawazo yako, na
Njia zako za ajabu.
Wanalia kwa furaha;
Mioyo ya shangwe.
Wataka watu wajue
Mambo wajuayo.
2. Mungu alikichagua
Kizazi kimsifu.
Nacho kipo sasa hivi,
Chafuata Mungu.
’Tumwa Mwaminifu,
Na “kondoo wengine”
Sasa wanakula,
Wakiongozwa na Yesu.
Washikamani wasifu
Kazi, jina lako.
Wabubujika kusema
Juu yako wewe.
3. Yehova mwema kwa wote;
Tuna uhakika.
Atawaokoa watu
—Kupitia Yesu.
Anavumilia;
Watu wake wajua.
Na tunashukuru
Ataka kuwa na sisi!
Yeye anatuinua
Na kutushibisha.
Twamubariki daima;
Tukisifu wema.