Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 30
  • Kuwajibu Washtaki Wake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuwajibu Washtaki Wake
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Kuwajibu Washtaki Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Uhusiano Kati ya Yesu na Baba Yake
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Sehemu Kuu ya Unabii Ilielekezwa Kwa Kristo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Kitabu Cha Biblia Namba 43—Yohana
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 30

Sura 30

Kuwajibu Washtaki Wake

WAKATI viongozi wa kidini Wayahudi wanapomshtaki Yesu juu ya kuvunja Sabato, yeye awajibu: “Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.”

Ijapokuwa madai ya Mafarisayo, kazi ya Yesu si ya namna ile iliyokatazwa na sheria ya Sabato. Kazi yake ya kuhubiri na kuponya ni mgawo kutoka kwa Mungu, na kwa kufuata kielelezo cha Mungu, yeye anaendelea kuifanya kila siku. Lakini, jibu lake linawakasirisha Wayahudi hata zaidi ya walivyokuwa hapo kwanza, na wanatafuta kumwua. Kwa nini?

Ni kwa sababu sasa si kwamba wanaamini tu Yesu anaivunja Sabato, bali wanaliona dai lake la kuwa Mwana wa kibinafsi wa Mungu kuwa kufuru. Lakini, Yesu haogopi na anawatolea jibu zaidi kuhusu uhusiano wake pamoja na Mungu uliopendelewa. “Baba ampenda Mwana,” anasema, “naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe.”

“Kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha,” Yesu aendelea, “vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.” Kwa kweli, tayari Mwana anafufua wafu kwa njia ya kiroho! “Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka,” Yesu asema, “amepita kutoka mautini kuingia uzimani.” Ndiyo, yeye aendelea: “Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.”

Ingawa kufikia wakati huu, hakuna kumbukumbu la kuonyesha kwamba Yesu amekwisha kufufua mtu yeyote kwa uhalisi kutoka kwa wafu, awaambia washtaki wake kwamba ufufuo wa wafu kwa njia hiyo halisi utatukia. “Msistaajabie maneno hayo,” asema, “kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka.”

Kufikia wakati huu, inaonekana kwamba Yesu hajapata kueleza hadharani daraka lake la maana sana katika kutimiza kusudi la Mungu kwa njia ya wazi na ya uthabiti mwingi hivyo. Lakini washtaki wa Yesu wana zaidi ya ushahidi wake mwenyewe kuhusu mambo haya. “Ninyi mlituma watu kwa Yohana,” Yesu awakumbusha, “naye akaishuhudia kweli.”

Miaka miwili tu kabla ya hapo, Yohana Mbatizaji aliwaambia viongozi hao wa kidini Wayahudi juu ya Yule mwenye kuja baada yake. Akiwakumbusha jinsi wakati mmoja walivyomheshimu sana Yohana ambaye sasa amefungwa gerezani, Yesu asema: “Nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda.” Yesu awakumbusha jambo hilo akiwa na matumaini ya kuwasaidia, ndiyo, kuwaokoa. Hata hivyo yeye hategemei ushahidi wa Yohana.

“Kazi hizo zenyewe ninazozitenda [kutia na mwujiza ambao ameufanya sasa hivi], zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.” Lakini zaidi ya hilo, Yesu aendelea kusema: “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia.” Mungu alitoa ushahidi juu ya Yesu, kwa kielelezo, wakati wa ubatizo wake, akisema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu.”

Kwa kweli, washtaki wa Yesu hawana udhuru wa kumkataa. Maandiko yale yale wanayodai kwamba wanayachunguza yanashuhudia juu yake! “Kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi,” Yesu amalizia, “kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?” Yohana 5:17-47; 1:19-27; Mathayo 3:17.

▪ Kwa nini kazi ya Yesu haivunji Sabato?

▪ Yesu aelezaje daraka lake la maana sana katika kusudi la Mungu?

▪ Ili kuthibitisha kwamba yeye ni Mwana wa Mungu, Yesu aonyesha ushahidi wa nani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki