Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • sp kur. 28-29
  • Wakati Ujao Mzuri Ajabu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakati Ujao Mzuri Ajabu
  • Roho za Wafu—Je! Zaweza Kukusaidia au Kukuumiza? Je Ziko Kweli?
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wafu Wataishi Tena!
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Kuponda Kichwa cha Nyoka
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
  • Yesu Ana Nguvu Kuliko Roho Waovu
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Ufundishaji wa Kimungu Dhidi ya Mafundisho ya Mashetani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Roho za Wafu—Je! Zaweza Kukusaidia au Kukuumiza? Je Ziko Kweli?
sp kur. 28-29

Wakati Ujao Mzuri Ajabu

Yesu akimtupa Shetani katika abiso

Karibuni Shetani na roho wake waovu watafungwa

Shetani na roho wake waovu hawatawadanganya wanadamu kwa muda mrefu. Tayari Yehova amewatupa kutoka mbinguni. (Ufunuo 12:9) Hivi karibuni, Mungu atachukua hatua tena dhidi ya Shetani na roho wake waovu. Katika maono kutoka kwa Mungu, mtume Yohana alisema hivi: “Nikamwona malaika akishuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa shimo refu lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamkamata yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, na kumfunga kwa miaka 1,000. Naye akamtupa katika shimo refu lisilo na mwisho akalifunga na kulitia muhuri juu yake, ili asipotoshe mataifa tena mpaka ile miaka 1,000 itakapokwisha.” (Ufunuo 20:1-3) Baadaye, Ibilisi na roho wake waovu wataangamizwa milele.—Ufunuo 20:10.

Watu wabaya duniani wataangamizwa pia.—Zaburi 37:9, 10; Luka 13:5.

Wafu Wataishi Tena!

Watu waliokuwa wamekufa wakikaribishwa katika dunia paradiso

Wafu watafufuliwa waishi tena duniani

Baada ya Shetani na roho wake waovu kuondolewa, Yehova atawaletea wanadamu baraka nyingi. Kumbuka kwamba wafu hawako hai, hawapo popote. Yesu alilinganisha kifo na usingizi—usingizi mzito usio na ndoto. (Yohana 11:11-14) Alifanya hivyo kwa sababu alijua kwamba wakati ungefika ambapo wale wanaolala katika kifo wangeamshwa waishi tena. Alisema: ‘Saa inakuja ambayo wote walio katika makaburi ya ukumbusho watatoka.’—Yohana 5:28, 29; Linganisha Matendo 24:15.

Watafufuliwa waishi hapa duniani. Badala ya matangazo ya vifo, kutakuwa na ripoti zenye kufurahisha za wale ambao wamefufuliwa! Itakuwa shangwe kama nini kuwakaribisha wapendwa wetu kutoka kaburini!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki