Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • rq somo la 11 kur. 22-23
  • Itikadi na Desturi Ambazo Hazimpendezi Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Itikadi na Desturi Ambazo Hazimpendezi Mungu
  • Mungu Anataka Tufanye Nini?
  • Habari Zinazolingana
  • Desturi Zinazopendwa na Watu Wengi Zinazomchukiza Mungu
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Ista au Ukumbusho—Ni Upi Unaopaswa Wewe Kuadhimisha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Amua Kumwabudu Mungu
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Kwa Nini Mashahidi wa Yehova Hawasherehekei Ista?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
Mungu Anataka Tufanye Nini?
rq somo la 11 kur. 22-23

Somo la 11

Itikadi na Desturi Ambazo Hazimpendezi Mungu

Ni aina zipi za itikadi na desturi zilizo mbaya? (1)

Je, Wakristo waamini kwamba Mungu ni Utatu? (2)

Kwa nini Wakristo wa kweli hawasherehekei Krismasi, Ista, au siku za kuzaliwa? (3, 4)

Je, wafu waweza kuwadhuru walio hai? (5)

Je, Yesu alikufa juu ya msalaba? (6)

Ni jambo la maana jinsi gani kumpendeza Mungu? (7)

1. Si itikadi na desturi zote zilizo mbaya. Lakini Mungu hazikubali ikiwa zinatokana na dini bandia au zinapingana na mafundisho ya Biblia.—Mathayo 15:6.

2. Utatu: Je, Yehova ni Utatu—watu watatu katika Mungu mmoja? La! Yehova, aliye Baba, ni “Mungu wa pekee wa kweli.” (Yohana 17:3; Marko 12:29) Yesu ni Mwana Wake mzaliwa wa kwanza, na anajitiisha kwa Mungu. (1 Wakorintho 11:3) Baba ni mkubwa zaidi ya Mwana. (Yohana 14:28) Roho takatifu si mtu; ni kani ya utendaji ya Mungu.—Mwanzo 1:2; Matendo 2:18.

3. Krismasi na Ista: Yesu hakuzaliwa Desemba 25. Alizaliwa Oktoba 1 hivi, wakati wa mwaka ambapo wachungaji waliweka makundi yao nje usiku. (Luka 2:8-12) Yesu hakuwaamuru Wakristo kamwe washerehekee kuzaliwa kwake. Badala ya hivyo, aliwaambia wanafunzi wake waadhimishe, au wakumbuke, kifo chake. (Luka 22:19, 20) Krismasi na desturi zayo hutokana na dini bandia za kale. Ndivyo ilivyo na desturi za Ista, kama vile utumizi wa mayai na sungura. Wakristo wa mapema hawakusherehekea Krismasi au Ista, wala Wakristo wa kweli leo hawazisherehekei.

4. Siku za Kuzaliwa: Misherehekeo ya siku ya kuzaliwa miwili pekee inayosimuliwa katika Biblia ilifanywa na watu ambao hawakumwabudu Yehova. (Mwanzo 40:20-22; Marko 6:21, 22, 24-27) Wakristo wa mapema hawakusherehekea siku za kuzaliwa. Desturi ya kusherehekea siku za kuzaliwa hutokana na dini bandia za kale. Wakristo wa kweli hutoa zawadi na huwa na pindi nzuri pamoja nyakati nyinginezo katika mwaka.

5. Kuhofu Wafu: Wafu hawawezi kufanya chochote wala kuhisi lolote. Sisi hatuwezi kuwasaidia, nao hawawezi kutuumiza. (Zaburi 146:4; Mhubiri 9:5, 10) Nafsi hufa; haiendelei kuishi baada ya kifo. (Ezekieli 18:4) Lakini nyakati nyingine malaika waovu, waitwao roho waovu, hujifanya kuwa roho za wafu. Desturi zozote zinazohusiana na kuhofu au kuabudu wafu ni mbaya.—Isaya 8:19.

6. Msalaba: Yesu hakufa juu ya msalaba. Alikufa juu ya nguzo, au mti. Neno la Kigiriki linalotafsiriwa “msalaba” katika Biblia nyingi lilimaanisha kipande kimoja tu cha mbao. Ishara ya msalaba hutokana na dini bandia za kale. Msalaba haukutumiwa wala kuabudiwa na Wakristo wa mapema. Kwa hiyo, je, wafikiri lingekuwa jambo la kufaa kuutumia msalaba katika ibada?—Kumbukumbu la Torati 7:26; 1 Wakorintho 10:14.

7. Huenda likawa jambo gumu sana kuacha baadhi ya itikadi na desturi hizi. Watu wa ukoo na marafiki huenda wakajaribu kukusadikisha usibadili itikadi zako. Lakini kumpendeza Mungu ni jambo la maana zaidi kuliko kuwapendeza wanadamu.—Mithali 29:25; Mathayo 10:36, 37.

[Picha katika ukurasa wa 22]

Mungu si Utatu

[Picha katika ukurasa wa 23]

Krismasi na Ista hutokana na dini bandia za kale

[Picha katika ukurasa wa 23]

Hakuna sababu ya kuabudu wafu au kuwahofu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki