Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • rq somo la 16 uku. 31
  • Uamuzi Wako wa Kumtumikia Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uamuzi Wako wa Kumtumikia Mungu
  • Mungu Anataka Tufanye Nini?
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Uko Tayari Kubatizwa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2020
  • Ubatizo na Uhusiano Wako Pamoja na Mungu
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
  • Je, Ninapaswa Kujiweka Wakfu kwa Mungu na Kubatizwa?
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Kufanye Kumtumikia Mungu Milele Kuwe Lengo Lako
    Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele
Pata Habari Zaidi
Mungu Anataka Tufanye Nini?
rq somo la 16 uku. 31

Somo la 16

Uamuzi Wako wa Kumtumikia Mungu

Ni lazima ufanye nini ili kuwa rafiki ya Mungu? (1, 2)

Unafanyaje wakfu wako kwa Mungu? (1)

Imekupasa ubatizwe wakati gani? (2)

Unaweza kupataje nguvu za kuendelea ukiwa mwaminifu kwa Mungu? (3)

1. Ili uwe rafiki ya Mungu, ni lazima upate ujuzi wa kutosha juu ya kweli ya Biblia (1 Timotheo 2:3, 4), uamini mambo ambayo umejifunza (Waebrania 11:6), utubu dhambi zako (Matendo 17:30, 31), na ugeuke katika mwendo wako wa maisha. (Matendo 3:19) Ndipo kumpenda kwako Mungu kutakusukuma ujiweke wakfu kwake. Hilo lamaanisha kwamba katika sala ya kibinafsi, ya faragha unamwambia kwamba unajitoa mwenyewe kwake ili kufanya mapenzi yake.—Mathayo 16:24; 22:37.

2. Baada ya wewe kujiweka wakfu kwa Mungu, wapaswa ubatizwe. (Mathayo 28:19, 20) Ubatizo unajulisha kila mtu kwamba umejiweka wakfu kwa Yehova. Kwa hiyo ubatizo ni wa wale tu walio na umri wa kutosha kufanya uamuzi wa kumtumikia Mungu. Mtu anapobatizwa, mwili wake mzima wapaswa uzamishwe majini kwa muda mfupi.a—Marko 1:9, 10; Matendo 8:36.

3. Baada ya wewe kujiweka wakfu, Yehova atakutazamia uishi kulingana na ahadi yako. (Zaburi 50:14; Mhubiri 5:4, 5) Ibilisi atajaribu kukuzuia usimtumikie Yehova. (1 Petro 5:8) Lakini mkaribie Mungu katika sala. (Wafilipi 4:6, 7) Jifunze Neno lake kila siku. (Zaburi 1:1-3) Shikamana kwa ukaribu na kutaniko. (Waebrania 13:17) Kwa kufanya hayo yote, utapata nguvu za kuendelea ukiwa mwaminifu kwa Mungu. Kwa umilele wote unaweza kufanya hivyo mambo ambayo Mungu anakutaka ufanye!

[Maelezo ya Chini]

a Funzo la kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele, au kinachofanana nacho kilichotangazwa na Watch Tower Bible and Tract Society, linapendekezwa katika kujitayarisha kwa ajili ya ubatizo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki