Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gf somo la 17 kur. 28-29
  • Ili Uendelee Kuwa Na Rafiki, Ni Lazima Uwe Rafiki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ili Uendelee Kuwa Na Rafiki, Ni Lazima Uwe Rafiki
  • Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
  • Habari Zinazolingana
  • Maajabu ya Mchanga
    Amkeni!—2003
  • Upendo wa Mungu Unadumu Milele
    Jinsi ya Kudumu Katika Upendo wa Mungu
  • Unajenga Juu ya Mchanga au Mwamba?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • “Kumpenda Mungu Humaanisha Hivi”
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
Pata Habari Zaidi
Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
gf somo la 17 kur. 28-29

SOMO LA 17

Ili Uendelee Kuwa Na Rafiki, Ni Lazima Uwe Rafiki

Urafiki hutegemea upendo. Kadiri ujifunzavyo juu ya Yehova, ndivyo utakavyozidi kumpenda. Uzidipo kumpenda Mungu, hamu yako ya kumtumikia itaongezeka pia. Hamu hiyo itakuchochea kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo. (Mathayo 28:19) Unaweza kuwa rafiki ya Mungu milele kwa kujiunga na familia yenye furaha ya Mashahidi wa Yehova. Unapaswa kufanya nini?

Ni lazima uonyeshe upendo wako kwa Mungu kwa kutii sheria zake. “Hivi ndivyo kumpenda Mungu humaanisha, kwamba tushike amri zake; na bado amri zake si zenye kulemea.”—1 Yohana 5:3.

Tenda mambo unayojifunza. Yesu alisimulia hadithi inayoonyesha jambo hilo. Mtu mwenye hekima alijenga nyumba yake juu ya mwamba. Mpumbavu naye akajenga nyumba yake juu ya mchanga. Dhoruba na mvua kubwa ilipokuja, nyumba iliyojengwa juu ya mwamba haikuanguka, lakini nyumba iliyojengwa juu ya mchanga ilianguka kwa kishindo kikubwa. Yesu alisema kuwa wale wanaosikia mafundisho yake na kuyatenda ni kama yule mtu mwenye hekima aliyejenga juu ya mwamba. Lakini wale wanaosikiliza mafundisho yake wala wasiyatende ni kama yule mpumbavu aliyejenga juu ya mchanga. Wewe ungependa kuwa mtu wa aina gani?—Mathayo 7:24-27.

Wakfu. Wakfu wamaanisha kwamba usali kwa Yehova na kumwambia kuwa unataka kufanya mapenzi yake milele. Kufanya mapenzi ya Mungu huonyesha kwamba wewe ni mwanafunzi wa Yesu Kristo.—Mathayo 11:29.

Ubatizo. “Ubatizwe na uoshe dhambi zako kwa kuitia jina lake.”—Matendo 22:16.

Mtumikie Mungu kikamili. “Lolote mnalofanya, lifanyeni kwa nafsi yote kama kwa Yehova, na si kwa wanadamu.”—Wakolosai 3:23.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki