Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yp2 uku. 50
  • Mfano wa Kuigwa—Yosefu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mfano wa Kuigwa—Yosefu
  • Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Habari Zinazolingana
  • “Ninawezaje Kufanya Ubaya Huu Mkubwa?”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Alikuwa Baba na Mume Aliyemwogopa Mungu
    Igeni Imani Yao
  • Mtumwa Aliyemtii Mungu
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • “Je, Mimi Niko Mahali pa Mungu?”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
Pata Habari Zaidi
Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
yp2 uku. 50

Mfano wa Kuigwa—Yosefu

Yosefu anakabili hali ngumu. Mke wa bwana wake amemsihi tena na tena afanye ngono naye. Sasa anajaribu tena! Lakini Yosefu anakataa. Anajibu kwa uthabiti. Anamwambia: “Ninawezaje kufanya ubaya huu mkubwa na kwa kweli nimtendee Mungu dhambi?” Mwanamke huyo anaposisitiza—hata kwa kumshi­ka—Yosefu haoni haya kukimbia. Anakimbia na kwenda nje! Yosefu anathibitisha kwamba ni mshikamanifu kiadili.—Mwanzo 39:7-12.

Wewe pia unaweza kujikuta katika hali kama hiyo ambayo mtu anataka utosheleze tamaa zako za ngono. Hutakataa tu kwa sababu unaweza kujidhibiti. Lakini utakataa kwa sababu unataka kumpendeza Muumba wako, Yehova Mungu. Yosefu alikuwa na tamaa za ngono, kama wewe. Hata hivyo, lilikuwa jambo lisilowazika kwake kutosheleza tamaa hizo kwa njia ambayo ingemkasirisha Muumba wake. Kwa njia hiyohiyo, unapaswa kusadiki kwamba uchafu wa kiadili unamkasirisha Mungu na mwishowe unaleta maumivu makali. Kwa hiyo, jitahidi kukuza na kudumisha ushikamanifu wa kiadili kama Yosefu alivyofanya.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki