Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yp2 uku. 134
  • Mfano wa Kuigwa—Wale Waebrania Watatu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mfano wa Kuigwa—Wale Waebrania Watatu
  • Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Habari Zinazolingana
  • Watahiniwa—Lakini Wadumisha Uaminifu Kwa Yehova!
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
  • Yehova Huthawabisha Imani na Ushujaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Jinsi Kitabu Cha Danieli Kinavyokuhusu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
Pata Habari Zaidi
Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
yp2 uku. 134

Mfano wa Kuigwa—Wale Waebrania Watatu

Hanania, Mishaeli, na Azaria wamesimama katika nchi tambarare ya Dura, karibu na Babiloni. Watu wote wanaowazunguka wanasujudia sanamu kubwa iliyo mbele yao. Ijapokuwa kuna mkazo mwingi kutoka kwa wenzao na vitisho kutoka kwa mfalme, vijana hao wanasimama imara. Kwa uthabiti, lakini kwa heshima wanamwambia Nebukadneza kwamba hawatabadili uamuzi wao wa kumtumikia Yehova.—Danieli 1:6; 3:17, 18.

Watatu hao walikuwa wangali vijana walipopelekwa uhamishoni Babiloni. Uaminifu wao wakiwa wangali vijana—kwa kukataa kula vyakula vilivyokuwa vimekatazwa katika Sheria ya Mungu—uliwatayarisha kukabili hali ngumu baadaye maishani mwao. (Danieli 1:6-20) Walikuwa wamejionea kwamba kumtii Yehova ndilo jambo la hekima maishani. Je, wewe pia umeazimia kushikamana na viwango vya Mungu hata ukabili mkazo kutoka kwa vijana wenzako? Ukijifunza kumtii Yehova ukiwa ungali kijana katika mambo ambayo huenda yakaonekana kuwa madogo, utakuwa tayari kuendelea kuwa mwaminifu ukikumbwa na hali ngumu zaidi baadaye maishani.—Methali 3:5, 6; Luka 16:10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki