Wimbo Na. 1
Sifa za Yehova
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova U Mungu daima,
U chanzo cha nuru na uzima.
Wasifiwa nazo kazi zako;
Zaonyesha nguvu zako.
2. Utawala wako wa haki.
Watufunza tufuate haki.
Tunapolisoma Neno lako,
Twaona hekima yako.
3. Kweli wewe ni mukarimu.
Upendo ni sifa yako kuu.
Jina lako, sifa zako pia,
Twafurahi kutangaza.
(Ona pia Zab. 36:9; 145:6-13; Yak. 1:17.)