Wimbo Na. 13
Sala ya Shukrani
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova Mungu wastahili sifa,
Ni wewe tunayekuimbia,
Nasi tunainama mbele zako
Twajiweka mikononi mwako.
Sisi ni watenda dhambi wanyonge;
Tunakuomba utusamehe.
Kwa damu ya Mwanao tusafishe
Na njia zako utufundishe.
2. Ni wenye shangwe unaoalika,
Nyuani mwako wamiminika.
Utuongoze kwalo Neno lako,
Na tukae hekaluni mwako.
Nguvu zako zisizo na kifani,
Hutoa watu wako gizani.
Ufalme wako tunautangaza,
Kwenye Ufalme macho twakaza.
3. Ulinzi wako tunafurahia;
Ibada yako twashangilia.
Ufalme wako wenye wema waja,
Kifo, huzuni, magonjwa, kwisha.
Yesu atauondoa uovu,
Kisha sote tupate wokovu.
Kwa shangwe ya ushindi tutaimba:
“Ee Yehova wastahili sifa!”
(Ona pia Zab. 65:2, 4, 11; Flp. 4:6.)