Wimbo Na. 24
Kaza Macho Kwenye Zawadi!
Makala Iliyochapishwa
1. Viziwi watasikia,
Vipofu nao waone,
Majangwa yatachanua,
Maji yatabubujika,
Walemavu wataruka,
Wapendwa wawe pamoja.
Utaona mambo hayo,
Ukitazama zawadi.
2. Wazee wawe vijana,
Mabubu wataongea,
Ardhi itazaa sana,
Mema yawepo milele,
Watoto washangilie,
Wote wawe na furaha.
Utaona ufufuo,
Ukitazama zawadi.
3. Kondoo, simba na dubu,
Wote watakula nyasi,
Na muvulana mudogo,
Atawaongoza wote.
Hakutakuwa machozi,
Woga, maumivu, kwisha.
Utaona hayo yote,
Ukitazama zawadi.
(Ona pia Isa. 11:6-9; 35:5-7; Yoh. 11:24.)