Wimbo Na. 32
Iweni Imara, Thabiti!
Makala Iliyochapishwa
1. Mataifa yana wasiwasi,
Mambo yanabadilika kasi.
Na tuwe thabiti na imara,
Tutende kwa busara.
(KORASI)
Imara tusimame;
Nyuma tusitazame.
Kwa utimilifu, Mungu tumusifu.
2. Mitego ya mufumo yazidi.
Tutashinda tukijitahidi.
Yaliyo kweli tukifuata,
Ulinzi tutapata.
(KORASI)
Imara tusimame;
Nyuma tusitazame.
Kwa utimilifu, Mungu tumusifu.
3. Ibada iwe ya moyo wote.
Tusilaumiwe kwa lolote.
Habari njema na tueneze.
Mungu tumupendeze.
(KORASI)
Imara tusimame;
Nyuma tusitazame.
Kwa utimilifu, Mungu tumusifu.
(Ona pia Luka 21:9; 1 Pet. 4:7.)