Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • bm seh. ya 14 uku. 17
  • Mungu Asema Kupitia Manabii Wake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mungu Asema Kupitia Manabii Wake
  • Biblia—Ina Ujumbe Gani?
  • Habari Zinazolingana
  • Manabii Waliotangaza Ujumbe Unaotuhusu
    Izingatie Siku ya Yehova Maishani
  • Nabii Aliye Uhamishoni Apata Maono ya Wakati Ujao
    Biblia—Ina Ujumbe Gani?
  • Masihi Afika
    Biblia—Ina Ujumbe Gani?
  • Je, Unabii wa Kimasihi Unathibitisha Kwamba Yesu Alikuwa Ndiye Masihi?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
Pata Habari Zaidi
Biblia—Ina Ujumbe Gani?
bm seh. ya 14 uku. 17
Nabii wa Mungu akiwasilisha ujumbe

Sehemu ya 14

Mungu Asema Kupitia Manabii Wake

Manabii wawekwa na Yehova watangaze ujumbe kuhusu hukumu, ibada safi, na tumaini la Kimasihi

WAKATI wa wafalme wa Israeli na Yuda, kulikuwa na kikundi fulani cha wanaume wa pekee—manabii. Walikuwa na imani ya pekee na ujasiri wa kutangaza ujumbe mbalimbali wa Mungu. Fikiria mambo manne makuu yaliyozungumziwa na manabii hao wa Mungu.

1. Kuharibiwa kwa Yerusalemu. Mapema sana, manabii wa Mungu—Isaya na Yeremia hasa—walianza kuonya kwamba Yerusalemu lingeharibiwa na kuachwa ukiwa. Walitangaza waziwazi ni kwa nini jiji hilo lilistahili hasira ya Mungu. Mazoea yake ya dini za uongo, ufisadi, na jeuri yalithibitisha dai lake la kumwakilisha Yehova kuwa la uwongo.—2 Wafalme 21:10-15; Isaya 3:1-8, 16-26; Yeremia 2:1–3:13.

2. Kurudishwa kwa ibada ya kweli. Baada ya miaka 70 ya uhamisho, watu wa Mungu waliachiliwa kutoka Babiloni. Walirudi katika makao yao yaliyokuwa ukiwa na kujenga upya hekalu la Yehova jijini Yerusalemu. (Yeremia 46:27; Amosi 9:13-15) Miaka 200 hivi mapema, Isaya alitabiri jina la mshindi—Koreshi—ambaye angeshinda Babiloni na kuwaruhusu watu wa Mungu warudishe tena ibada safi. Isaya hata alieleza waziwazi jinsi ambavyo Koreshi angefanya hivyo.—Isaya 44:24–45:3.

Wayahudi waliokuwa uhamishoni wakitoka Babiloni na kurudi Yerusalemu

3. Kufika kwa Masihi na mambo yaliyompata. Masihi angezaliwa katika mji wa Bethlehemu. (Mika 5:2) Angekuwa mnyenyekevu, angeingia Yerusalemu akiwa amepanda punda. (Zekaria 9:9) Ijapokuwa alikuwa mpole na mwenye fadhili, hangependwa na wengi, badala yake wengi wangemkataa. (Isaya 42:1-3; 53:1, 3) Angeuawa kikatili. Je, huo ndio ungekuwa mwisho wake? Hapana, kwa kuwa dhabihu yake ingewezesha msamaha wa dhambi za watu wengi. (Isaya 53:4, 5, 9-12) Ufufuo wake tu ndio ungewezesha hilo.

4. Utawala wa Masihi juu ya dunia. Wanadamu wasio wakamilifu hawawezi kujitawala wenyewe kwa amani, lakini Mfalme wa Kimasihi angeitwa Mkuu wa Amani. (Isaya 9:6, 7; Yeremia 10:23) Chini ya utawala wake, kungekuwa na amani kati ya wanadamu wote na pia wanyama. (Isaya 11:3-7) Magonjwa hayatakuwako. (Isaya 33:24) Hata kifo kitamezwa milele. (Isaya 25:8) Wakati wa utawala wa Masihi, wafu watafufuliwa waishi duniani.—Danieli 12:13.

—Inatoka kwenye Isaya, Yeremia, Danieli, Amosi, Mika, na Zekaria.

  • Manabii wa Mungu walitangaza ujumbe gani?

  • Manabii walitabiri kuharibiwa na kujengwa upya kwa Yerusalemu jinsi gani?

  • Manabii wa Yehova walisema nini kuhusu Masihi na mambo ambayo yangempata?

  • Manabii walifafanua jinsi gani utawala wa Masihi juu ya dunia?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki