Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yc somo la 5 kur. 12-13
  • Samweli aliendelea kufanya mambo mazuri

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Samweli aliendelea kufanya mambo mazuri
  • Wafundishe Watoto Wako
  • Habari Zinazolingana
  • Samweli Alifanya Yaliyo Sawa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Mvulana Mdogo Anamtumikia Mungu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • ‘Aliendelea Kukua Akiwa na Yehova’
    Igeni Imani Yao
  • ‘Aliendelea Kukua Akiwa na Yehova’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Wafundishe Watoto Wako
yc somo la 5 kur. 12-13

SOMO LA 5

Samweli Aliendelea Kufanya Mambo Mazuri

Tangu alipokuwa mtoto mdogo sana, Samweli aliishi na kufanya kazi katika maskani, mahali ambapo watu walienda ili kumwabudu Yehova. Je, unajua jinsi ambavyo Samweli alianza kuishi katika maskani? Kwanza kabisa, ngoja tuanze kwa kujifunza jambo fulani kuhusu mama ya Samweli, aliyeitwa Hana.

Kwa muda mrefu sana, Hana alitamani kupata mtoto lakini hakupata. Kwa hiyo, alisali kwa Yehova na kumwomba amsaidie ili apate mtoto. Alimwahidi Yehova kwamba ikiwa atapata mtoto, basi atampeleka katika maskani ili aishi na kufanya kazi huko. Yehova alijibu sala yake, kwa hiyo akapata mtoto wa kiume. Akamwita jina lake Samweli. Na kama vile alivyoahidi, Hana akampeleka Samweli katika maskani ili amtumikie Mungu huko, wakati huo Samweli alikuwa na miaka mitatu au minne.

Eli alikuwa kuhani mkuu katika maskani hiyo. Watoto wake wawili wa kiume walifanya kazi katika maskani pia. Kumbuka kwamba, maskani ilikuwa nyumba ya Mungu kwa ajili ya ibada, na watu walipaswa kufanya mambo mazuri katika maskani. Lakini watoto wa Eli walikuwa wakifanya mambo mabaya sana. Samweli aliona mambo waliyokuwa wakifanya. Je, Samweli alifanya mambo mabaya kama watoto wa Eli walivyofanya?— Hapana, aliendelea kufanya mambo mazuri, kama alivyofundishwa na wazazi wake.

Unafikiri Eli alipaswa kuwafanya nini watoto wake?— Alipaswa kuwaadhibu watoto wake, na kuwaondoa katika nyumba ya Mungu ili wasifanye kazi tena katika nyumba hiyo. Lakini Eli hakufanya hivyo, kwa hiyo Yehova alimkasirikia sana Eli pamoja na watoto wake wawili. Yehova akaamua kuwaadhibu.

Kijana Samweli akizungumza na Kuhani Mkuu Eli

Samweli alifikisha ujumbe wa Yehova kwa Eli

Siku moja usiku Samweli alipokuwa amelala, alimsikia mtu fulani akimwita: ‘Samweli!’ Akakimbia hadi alipokuwa Eli, lakini Eli akamwambia: ‘Mimi sikukuita.’ Jambo hilo likatokea mara mbili zaidi. Baada ya kuitwa mara ya tatu, Eli akamwambia Samweli kwamba ikiwa atasikia sauti ikimwita tena, anapaswa kusema: ‘Tafadhali, Yehova, sema; ninakusikiliza.’ Basi Samweli akafanya kama alivyoambiwa na Eli. Kisha Yehova akamwambia hivi Samweli: ‘Mwambie Eli kwamba nitaiadhibu familia yake kwa sababu ya mambo mabaya ambayo wamefanya.’ Je, unafikiri ilikuwa rahisi kwa Samweli kumwambia Eli ujumbe huo?— Hapana, haikuwa rahisi. Hata hivyo, licha ya kwamba Samweli aliogopa, alifanya jambo ambalo Yehova alimwambia afanye. Jambo hilo lilitimia kama Yehova alivyosema. Watoto wawili wa Eli waliuawa, na kisha Eli akafa pia.

Samweli ametuwekea mfano mzuri wa kuiga. Alifanya mambo mazuri licha ya kwamba aliwaona watu wengine wakifanya mambo mabaya. Namna gani wewe? Je, utakuwa kama Samweli na kuendelea kufanya mambo mazuri? Ukifanya hivyo, utamfurahisha Yehova na wazazi wako pia.

SOMA KATIKA BIBLIA YAKO

  • 1 Samweli 2:22-26; 3:1-21

MASWALI:

  • Mama yake Samweli alimwahidi Yehova jambo gani?

  • Samweli aliona watoto wa Eli wakifanya mambo gani katika maskani?

  • Yehova alimwambia Samweli afanye nini?

  • Kwa nini Samweli ni mfano mzuri wa kuigwa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki