Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yc somo la 12 kur. 26-27
  • Mpwa wa Paulo alikuwa jasiri

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mpwa wa Paulo alikuwa jasiri
  • Wafundishe Watoto Wako
  • Habari Zinazolingana
  • Mwana wa Dada ya Paulo Amwokoa Asiuawe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • “Nisikilizeni Ninapojitetea”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
  • Uwe Jasiri​—Yehova Ni Msaidizi Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2020
  • Piga Mbiu ya Ufalme wa Yehova kwa Ujasiri!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Wafundishe Watoto Wako
yc somo la 12 kur. 26-27
Mpwa wa Paulo akizungumza na kamanda wa jeshi

SOMO LA 12

Mpwa wa Paulo Alikuwa Jasiri

Sasa ngoja tujifunze kuhusu kijana fulani ambaye aliokoa maisha ya mjomba wake. Mjomba wa kijana huyo alikuwa mtume Paulo. Hatujui jina la kijana huyo, lakini tunajua kwamba alitenda tendo fulani la ujasiri sana. Je, ungependa kujua tendo hilo?—

Paulo alikuwa amefungwa gerezani katika jiji la Yerusalemu. Alikuwa amekamatwa kwa sababu ya kuhubiri kuhusu Yesu. Watu fulani wabaya walimchukia Paulo, kwa hiyo wakapanga njama mbaya sana. Wakaambiana hivi: ‘Ngoja tumwombe kamanda wa jeshi awaagize askari wake wampeleke Paulo mahakamani. Halafu tutajificha pembeni mwa barabara, kisha wakati Paulo anapita, tutamuua!’

Mtume Paulo akimsikiliza mpwa wake gerezani

Mpwa wa Paulo alimwambia Paulo na kamanda wa jeshi kuhusu njama fulani mbaya sana

Mpwa wa Paulo alisikia kuhusu njama hiyo. Angefanya nini? Alienda gerezani na kumwambia Paulo kuhusu njama hiyo. Mara moja, Paulo akamwambia aende kwa kamanda wa jeshi ili amwambie kuhusu njama hiyo mbaya sana. Je, unafikiri ilikuwa rahisi kwa mpwa wa Paulo kumfikia kamanda ili amwambie kuhusu njama hiyo?— Hapana, kwa sababu kamanda huyo alikuwa mtu mwenye cheo. Lakini mpwa wa Paulo alikuwa jasiri, hivyo akaenda kwa kamanda na kumwambia kuhusu njama hiyo.

Kamanda huyo alijua jambo alilohitaji kufanya. Aliandaa wanajeshi 500 ili wamlinde Paulo! Akawaambia wampeleke Paulo katika jiji la Kaisaria usiku huohuo. Je, Paulo alifika akiwa salama?— Bila shaka, watu hao wabaya hawakuweza kumshambulia! Njama yao mbaya iligonga mwamba.

Unajifunza jambo gani katika hadithi hii?— Wewe pia, unaweza kuwa jasiri kama mpwa wa Paulo. Tunahitaji kuwa jasiri tunapoongea na watu wengine kuhusu Yehova. Je, utakuwa jasiri na kuendelea kuongea na watu kuhusu Yehova?— Ukifanya hivyo, huenda ukaokoa maisha ya mtu mwingine.

SOMA KATIKA BIBLIA YAKO

  • Matendo 23:12-24

  • Mathayo 24:14; 28:18-20

  • 1 Timotheo 4:16

MASWALI:

  • Watu fulani wabaya walipanga kumfanya nini Paulo?

  • Mpwa wa Paulo alifanya nini? Kwa nini jambo hilo lilikuwa tendo la ujasiri?

  • Wewe unawezaje kuwa jasiri kama mpwa wa Paulo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki