Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ypq swali 7 kur. 21-23
  • Nifanye Nini Ninaposhinikizwa Kufanya Ngono?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nifanye Nini Ninaposhinikizwa Kufanya Ngono?
  • Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Ngono Itafanya Urafiki Wetu Uwe Mzuri Zaidi?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Je, Ngono Itaboresha Uhusiano Wetu?
    Amkeni!—2010
  • Ninaweza Kufanya Nini Ili Kupinga Shinikizo la Kufanya Ngono?
    Vijana Huuliza
  • Nitawaelezaje Wengine Msimamo Wangu Kuhusu Ngono?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
ypq swali 7 kur. 21-23
Msichana akikataa kutongozwa

SWALI LA 7

Nifanye Nini Ninaposhinikizwa Kufanya Ngono?

KWA NINI NI MUHIMU

Maamuzi yako kuhusu ngono yanaathiri sana wakati wako ujao.

WEWE UNGEFANYA NINI?

Fikiria hali hii: Heather amekuwa na urafiki na Mike kwa miezi miwili tu, lakini anahisi kana kwamba amemfahamu maisha yake yote. Wao huandikiana ujumbe mfupi nyakati zote, wanazungumza kwa saa nyingi kwenye simu, na hata mmoja akianza sentensi mwenzake anaweza kuimalizia! Lakini sasa Mike anataka mengi zaidi kuliko mazungumzo.

Katika kipindi cha miezi miwili ambayo imepita, Mike na Heather hawajafanya lolote ila kubusu na kushikana mikono. Heather hataki kufanya zaidi ya hayo. Lakini pia hataki kumpoteza Mike. Hakuna mtu mwingine anayemfanya ajihisi kuwa mrembo sana na wa pekee kama Mike anavyomfanya ahisi. ‘Isitoshe,’ Heather anawaza, ‘Mimi na Mike tunapendana . . . ’

Ikiwa una umri wa kutosha kuanzisha urafiki wa karibu na mtu wa jinsia tofauti na ujikute katika hali ya Heather, utafanya nini?

TUA NA UFIKIRI!

Vazi linatumiwa kama kitambaa cha kufanya usafi

Ngono ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa ajili ya watu waliofunga ndoa tu. Kufanya ngono kabla ya ndoa ni kutumia vibaya zawadi hiyo. Ni kama kuchukua vazi maridadi ulilopewa na kulitumia kama kitambaa cha kufanya usafi

Ukipuuza sheria za asili, kama vile ukijirusha kutoka juu sana na ujaribu kuruka kama ndege, utaumia. Ndivyo itakavyokuwa pia ukipuuza sheria za maadili, kama ile inayosema: “Mjiepushe na uasherati.”—1 Wathesalonike 4:3.

Kutotii amri hiyo kuna madhara gani? Biblia inasema hivi: “Yeye aliye na mazoea ya kufanya uasherati anautendea dhambi mwili wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 6:18) Je, hilo ni kweli?

Wachunguzi wamegundua kwamba vijana wengi ambao wamefanya ngono kabla ya ndoa wamepatwa na angalau moja kati ya mambo yafuatayo.

  • MAJUTO. Vijana wengi ambao wamefanya ngono kabla ya ndoa wanasema kwamba walijuta baadaye.

  • KUTOAMINIANA. Baada ya kufanya ngono, kila mmoja huanza kujiuliza, ‘Amefanya ngono na nani mwingine?’

  • KUTOTIMIZWA KWA MATARAJIO. Tamaa ya moyoni ya wasichana wengi ni kuwa na mtu atakayewalinda, si kuwatumia vibaya. Nao wavulana wengi hawavutiwi sana na msichana baada ya kufanya ngono naye.

  • Jambo kuu: Ukijihusisha katika ngono kabla ya ndoa, utajishushia heshima kwa kupoteza kitu chenye thamani sana. (Waroma 1:24) Mwili wako ni wenye thamani sana, hupaswi kuutumia ovyoovyo!

Onyesha kwamba una msimamo thabiti kwa ‘kujiepusha na uasherati.’ (1 Wathesalonike 4:3) Kisha ikiwa utafunga ndoa siku moja, unaweza kufanya ngono. Nawe utaifurahia kabisa, bila wasiwasi, majuto, wala mahangaiko ambayo mara nyingi watu hupata wanapojihusisha katika ngono kabla ya ndoa.—Methali 7:22, 23; 1 Wakorintho 7:3.

UNA MAONI GANI?

  • Je, kweli mtu anayekupenda kikweli anaweza kuhatarisha hali yako ya kimwili na ya kihisia?

  • Mtu anayekujali kikweli anaweza kukushawishi uhatarishe uhusiano wako pamoja na Mungu?—Waebrania 13:4.

KWA AJILI YA WASICHANA

Msichana akiwa ameketi huku akifikiri

Wavulana kadhaa wamesema kwamba hawawezi kumwoa msichana ambaye wamefanya naye ngono. Kwa nini? Kwa sababu wangependa mtu aliye safi!

Je, hilo linakushangaza, na labda hata kukuudhi? Basi kumbuka jambo hili: Sinema na televisheni hutukuza ngono kati ya vijana na kuifanya ionekane kuwa burudani isiyodhuru au kwamba ndio upendo wa kweli.

Lakini usidanganyike! Wale wanaojaribu kukushawishi ufanye ngono kabla ya ndoa wanatafuta tu faida zao wenyewe.—1 Wakorintho 13:4, 5.

KWA AJILI YA WAVULANA

Mvulana akiwa ameketi huku akifikiri

Ikiwa una urafiki wa karibu na msichana, jiulize, ‘Je, kweli ninamjali?’ Ikiwa jibu lako ni ndiyo, unaweza kuonyeshaje unamjali? Kwa kuwa na nguvu za kushikamana na sheria za Mungu, hekima ya kuepuka hali zenye kushawishi, na upendo utakaokusaidia kuhangaikia faida zake.

Ikiwa una sifa kama hizo, basi yaelekea msichana huyo atahisi kama alivyohisi msichana Mshulami mwenye maadili mazuri aliyesema: “Mpenzi wangu ni wangu nami ni wake.” (Wimbo wa Sulemani 2:16) Kwa ufupi, atakupenda hata zaidi!

MAPENDEKEZO

Mtu akijaribu kukushurutisha ufanye naye ngono kwa kukuambia, “Ikiwa unanipenda, utanikubalia,” mjibu hivi kwa uthabiti, “Ikiwa kweli unanipenda, huwezi kuniomba nifanye hivyo!”

Inapohusu mwenendo wako pamoja na watu wa jinsia tofauti, sheria nzuri ya kufuata ni hii: Ikiwa ni jambo ambalo hungependa wazazi wako waone ukifanya, basi hupaswi kulifanya.

HATUA ZA KUCHUKUA

  • Utatendaje mtu akikuomba ufanye naye ngono?

  • Ni hali zipi zitakazofanya iwe vigumu zaidi kwako kukataa?

  • Utaepukaje hali hizo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki