Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ypq swali 9 kur. 27-29
  • Je, Niamini Mageuzi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Niamini Mageuzi?
  • Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
  • Habari Zinazolingana
  • Uumbaji au Mageuzi?—Sehemu ya 2: Kwa Nini Uchunguze Nadharia ya Mageuzi?
    Vijana Huuliza
  • Uumbaji au Mageuzi?—Sehemu ya 1: Kwa Nini Nimwamini Mungu?
    Vijana Huuliza
  • Je, Fundisho la Mageuzi Linapatana na Biblia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Ninaweza Kuiteteaje Imani Yangu Katika Uumbaji?
    Amkeni!—2006
Pata Habari Zaidi
Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
ypq swali 9 kur. 27-29
Vijana wakitazama fuvu darasani

SWALI LA 9

Je, Niamini Mageuzi?

KWA NINI NI MUHIMU

Ikiwa mageuzi ni nadharia ya kweli, basi maisha hayana kusudi la kudumu. Ikiwa uumbaji ni fundisho la kweli, basi tunaweza kupata majibu yenye kuridhisha kwa maswali kuhusu uhai na wakati ujao.

WEWE UNGEFANYA NINI?

Fikiria hali hii: Alex amechanganyikiwa. Sikuzote amekuwa akiamini kwamba kuna Mungu na pia anaamini katika uumbaji. Lakini leo mwalimu wake wa biolojia amesisitiza kwamba nadharia ya mageuzi ni jambo hakika linalotegemea utafiti unaoaminika wa kisayansi. Alex hataki kuonekana mpumbavu. Anajiambia: ‘Kwa kweli, ikiwa wanasayansi wamethibitisha kwamba nadharia ya mageuzi ni ya kweli, mimi ni nani niwapinge?’

Ikiwa ungekuwa Alex, ungekubali mageuzi kwa sababu tu vitabu vinasema ni jambo hakika?

TUA NA UFIKIRI!

Mara nyingi watu wanaoamini uumbaji na wale wanaoamini mageuzi wote husema tu kile wanachoamini bila kujua kwa nini wanaamini jambo hilo.

  • Watu fulani huamini uumbaji kwa sababu hivyo ndivyo wamefundishwa kanisani.

  • Watu wengi huamini mageuzi kwa sababu hivyo ndivyo wamefundishwa shuleni.

MASWALI SITA YA KUFIKIRIA

Biblia inasema hivi: “Kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yeye aliyevijenga vitu vyote ni Mungu.” (Waebrania 3:4) Je, hilo ni wazo linalopatana na akili?

Kijana akitazama nyumba

Kudai kwamba hakuna Muumba ni wazo la kipumbavu sawa tu na kudai kwamba nyumba hii haikujengwa na mtu

DAI: Kila kitu ulimwenguni kilitokea kwa sababu ya mlipuko mkubwa uliotokea ghafla bila kutarajia.

1. Ni nani au ni nini kilichosababisha mlipuko huo?

2. Ni jambo gani linalopatana na akili zaidi, kwamba kila kitu kilijitokeza chenyewe au kwamba kila kitu kilitokana na mtu fulani?

DAI: Wanadamu walitokana na wanyama.

3. Ikiwa wanadamu walitokana na wanyama, kwa mfano kama vile sokwe, kwa nini kuna tofauti kubwa sana kati ya uwezo wa akili wa wanadamu na ule wa sokwe?

4. Kwa nini hata namna za “msingi” kabisa za uhai ni tata sana?

DAI: Nadharia ya mageuzi ni jambo lililothibitishwa.

5. Je, yule anayedai hivyo, amechukua hatua ya kuchunguza uthibitisho huo yeye mwenyewe?

6. Ni watu wangapi wanaoamini mageuzi kwa sababu tu wameambiwa kwamba watu wote wenye akili wanaamini hivyo pia?

“Ikiwa ungekuwa ukitembea msituni kisha uone nyumba maridadi, je, ungejiambia: ‘Ajabu sana. Lazima hii miti iwe ilianguka kwa mpangilio kisha ikatokeza nyumba hii.’ Huwezi kufikiri hivyo! Haipatani na akili kufikiri hivyo. Kwa hiyo, kwa nini tuamini kwamba kila kitu katika ulimwengu kilijitokeza chenyewe?”—Julia.

“Wazia ikiwa mtu angekuambia kwamba mlipuko ulitokea katika kiwanda cha uchapishaji kisha wino ukatapakaa ukutani na kwenye dari na kutokeza kamusi nzuri na iliyo sahihi. Ungemwamini?”—Gwen.

KWA NINI UMWAMINI MUNGU?

Biblia inakutia moyo utumie ‘nguvu zako za kufikiri.’ (Waroma 12:1) Hilo linamaanisha kwamba imani yako kumwelekea Mungu haipaswi kutegemea tu

  • HISIA (Ninahisi kwamba kuna mtu mwenye nguvu zinazozidi zile za kibinadamu)

  • MAONI YA WENGINE (Ninaishi katika jamii inayopenda mambo ya dini)

  • KUSHINIKIZWA (Wazazi wangu walinifundisha nimwamini Mungu —kwa hiyo siwezi kuamini kitu tofauti)

Badala yake, unapaswa kuwa na sababu za msingi za kukufanya uamini jambo hilo.

“Ninapokuwa darasani nikimsikiliza mwalimu akieleza jinsi miili yetu inavyofanya kazi, nina uhakika kwamba kuna Mungu. Kila sehemu ya mwili ina kazi yake, kutia ndani vitu vidogo sana, na mifumo mbalimbali hufanya kazi bila sisi wenyewe kujua. Kwa kweli mwili wa mwanadamu unastaajabisha sana!”—Teresa.

“Ninapoona jengo refu sana, meli, au gari, mimi hujiuliza, ‘Ni nani aliyetengeneza kitu hiki?’ Gari hutengenezwa na watu wenye akili sana kwa sababu vitu vidogo-vidogo sana lazima vifanye kazi vizuri ili gari liweze kusonga. Ikiwa lazima gari libuniwe na mtu fulani, basi lazima mwanadamu awe alibuniwa na mtu fulani pia.” —Richard.

“Kadiri nilivyojifunza sayansi, ndivyo nilivyoshindwa kuamini mageuzi. . . . Kwa maoni yangu, mtu anahitaji kuwa na ‘imani’ zaidi kuamini mageuzi kuliko kuamini kuna Muumba.”—Anthony.

MAMBO YA KUFIKIRIA

Ingawa wanasayansi wamefanya utafiti kwa miaka mingi kuhusu nadharia ya mageuzi, bado hawajapata ufafanuzi hususa ambao wanasayansi wote wanakubaliana nao. Ikiwa wanasanyansi hawakubaliani kuhusu nadharia ya mageuzi, na wao ndio wataalamu, je, ni kosa kutilia shaka nadharia hiyo?

HATUA ZA KUCHUKUA

  • Wazia kwamba mwanafunzi mwenzako amekuambia: “Siamini kuna Mungu. Wewe unaamini nini?” Hebu andika utamjibuje.

JIFUNZE ZAIDI!

Vijana Wenzako Wanasema nini—Kumwanimi Mungu

Tazama video Vijana Wenzako Wanasema Nini—Kumwamini Mungu kwenye www.jw.org/sw. (Tafuta kwenye MAFUNDISHO YA BIBLIA > MATINEJA)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki