WIMBO NA. 13
Kristo, Kielelezo Chetu
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova ni mwenye,
upendo na mwema,
Katoa Mwana wake wa Pekee
Awe mwanadamu,
kusudi tumwige
Tulitukuze jina la Mungu
2. Neno la Yehova,
lilimwimarisha.
Kwake lilikuwa kama chakula.
Kawa na hekima,
ufahamu pia,
Katuachia kielelezo
3. Kama Yesu Kristo,
tumsifu Mungu
Tuzifuate hatua za Yesu.
Tumwige daima,
maishani mwetu.
Tutapata kibali cha Mungu.
(Ona pia Yoh. 8:29; Efe. 5:2; Flp. 2:5-7.)