WIMBO NA. 40
Sisi Ni wa Nani?
Makala Iliyochapishwa
1. Wewe ni wa nani?
Unamtii nani?
Yule unayemwinamia,
Huyo ndiye Mungu wako.
Miungu wawili,
Huwezi kuabudu.
Hatimaye uamuzi wako,
Wategemea moyo.
2. Wewe ni wa nani?
Utamtii nani?
Yupo wa kweli, yupo mwongo.
Basi amua mwenyewe.
Je, ni Kaisari
Utakayemtii?
Ama Yehova Mungu wa kweli
Na kumtumikia?
3. Mimi ni wa nani?
Yehova nitatii.
Nitamtumikia Yeye,
Niweke nadhiri zangu.
Alininunua,
Nishikamane naye.
Nitayafanya mapenzi yake;
Nitamsifu Yeye.
(Ona pia Yos. 24:15; Zab. 116:14, 18; 2 Tim. 2:19.)