WIMBO NA. 83
“Nyumba kwa Nyumba”
Makala Iliyochapishwa
1. Kila mlango, kila nyumba,
Neno twaeneza.
Mijini na vijijini,
Kondoo walishwa.
Ufalme unatawala,
Ni habari njema.
Wazee hata vijana,
Wanazitangaza.
2. Kila mlango, kila nyumba,
Wokovu twataja.
Wanaomwita Yehova,
Wataokolewa.
Wataitaje jina la
Wasiyemjua?
Kila mlango, kila nyumba,
Jina twatangaza.
3. Kila mlango, basi twende,
Habari tweneze.
Wakubali, wakatae,
Wajiamulie.
Angalau jina Lake,
Twatangaza kote.
Kila mlango basi twende,
Kondoo tupate.
(Ona pia Mdo. 2:21; Rom. 10:14.)