WIMBO NA. 84
Tumejitoa Kutumikia
Makala Iliyochapishwa
1. Baba yetu, anajua.
Kuna shangwe kutumika.
Anatupa fursa nyingi.
Tupanue utumishi.
(KORASI)
Twafanya twezayo
Kwa nguvu zote
Kwenye uhitaji, twaenda.
Tumejitoa.
2. Kuna mengi ya kufanya
Twawajali watu wote.
Na wakati wa majanga,
Twaandaa misaada.
(KORASI)
Twafanya twezayo
Kwa nguvu zote
Kwenye uhitaji, twaenda.
Tumejitoa.
3. Nazo kazi za ujenzi
Twashiriki kwa bidii.
Lugha mpya twajifunza
Tufundishe wote kweli.
(KORASI)
Twafanya twezayo
Kwa nguvu zote
Kwenye uhitaji, twaenda.
Tumejitoa.
(Ona pia Yoh. 4:35; Mdo. 2:8; Rom. 10:14.)