WIMBO NA. 102
“Mwasaidie Walio Dhaifu”
Makala Iliyochapishwa
1. Kila mmoja wetu
Dhambi hutenda.
Hata hivyo, Yehova
Anatupenda.
Ni mwenye rehema,
Twataka kumwiga.
Ambao ni dhaifu,
Tusaidie.
2. Imani ya wengine,
Imepungua.
Kupitia maneno
Tuwafariji.
Walio dhaifu
Ni wa Mungu pia.
Tuwahangaikie,
Waimarike.
3. Tusiwe wachambuzi,
Tusiwakwaze.
Tuonyeshe fadhili,
Waimarike.
Tuwe na bidii,
Moyo tuwatie;
Na tuwategemeze,
Wafarijike.
(Ona pia Isa. 35:3, 4; 2 Kor. 11:29; Gal. 6:2.)