WIMBO NA. 116
Nguvu za Fadhili
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova Mungu tunakusifu,
Kwa hekima yako.
Japo ukuu, na nguvu zako,
Watuonyesha fadhili.
2. Mwanao Yesu akaribisha,
Wataabikao.
Waichukue nira laini,
Wapate kuburudishwa.
3. Yehova Mungu na Yesu Kristo,
Tuwaige wao.
Katika yote tuyafanyayo,
Na tuonyeshe fadhili.
(Ona pia Mika 6:8; Mt. 11:28-30; Kol. 3:12; 1 Pet. 2:3.)