WIMBO NA. 142
Kushikilia Tumaini Letu
Makala Iliyochapishwa
1. Kwa karne nyingi watu wako gizani.
Kazi zao ubatili mtupu.
Inazidi kuonekana wazi:
Kujiokoa hawawezi.
(KORASI)
Mwimbieni na kushangilia!
Ufalme wake unakaribia.
Uovu ataufutilia;
Tumaini letu twashikilia.
2. ‘Siku ya Mungu iko karibu sana! ’
Tusilie, ‘Jamani hadi lini? ’
Karibuni tutapata uhuru.
Yehova Mungu msifuni.
(KORASI)
Mwimbieni na kushangilia!
Ufalme wake unakaribia.
Uovu ataufutilia;
Tumaini letu twashikilia.
(Ona pia Zab. 27:14; Mhu. 1:14; Yoe. 2:1; Hab. 1:2, 3; Rom. 8:22.)