SOMO LA 5
Kusoma kwa Usahihi
1 Timotheo 4:13
MUHTASARI: Soma kwa sauti kile hasa kilichoandikwa kwenye ukurasa.
JINSI YA KUFANYA HIVYO:
Tayarisha vizuri. Elewa kusudi la kuandikwa kwa simulizi hilo. Jizoeze kusoma mafungu ya maneno, si neno mojamoja. Epuka kuongeza, kurukaruka, au kubadilisha maneno. Zingatia alama za vituo.
Tamka kila neno kwa usahihi. Ikiwa hujui jinsi neno linavyotamkwa, liangalie katika kamusi, sikiliza rekodi ya chapisho lililosomwa, au uombe msaada kutoka kwa msomaji mzuri.
Zungumza waziwazi. Tamka maneno waziwazi, inua kichwa chako na ufumbue kabisa kinywa unapoongea. Jitahidi kutamka kila silabi.