Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • th somo la 8 uku. 11
  • Mifano Inayofundisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mifano Inayofundisha
  • Boresha Uwezo Wako wa Kusoma na Kufundisha
  • Habari Zinazolingana
  • “Hakuwa Akisema Nao Bila Mfano”
    ‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
  • “Bila Kielezi Hakuwa Akisema Nao”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Fundisha kwa Ufahamu Wenye Kina na Ushawishi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Mwige Mwalimu Mkuu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
Pata Habari Zaidi
Boresha Uwezo Wako wa Kusoma na Kufundisha
th somo la 8 uku. 11

SOMO LA 8

Mifano Inayofundisha

Andiko lililotajwa

Mathayo 13:34, 35

MUHTASARI: Boresha ufundishaji wako kwa kutumia mifano rahisi inayowavutia wasikilizaji wako na kufundisha mambo muhimu.

JINSI YA KUFANYA HIVYO:

  • Chagua mifano rahisi. Kama Yesu, tumia mambo ya kawaida kuelezea mambo muhimu, na mambo rahisi kuelezea mambo magumu. Usiongeze habari zisizohitajika ambazo zitafanya mfano uwe mgumu. Hakikisha kwamba kila sehemu ya mfano wako inahusiana kikweli na somo unalofundisha ili wasikilizaji wasikengeushwe na sehemu zisizopatana.

    Dokezo linalofaa

    Uwe macho. Angalia mambo yanayokuzunguka, jifunze machapisho ya Kikristo, na uwasikilize walimu stadi. Unapofanya hivyo, tafuta mifano unayoweza kutumia kuboresha ufundishaji wako. Hifadhi mifano hiyo katika faili.

  • Fikiria mambo yatakayowanufaisha wasikilizaji wako. Chagua mifano inayohusisha utendaji na mapendezi ya wasikilizaji wako. Uwe mwangalifu mifano yako isiwaaibishe au kuwakasirisha.

  • Fundisha jambo kuu. Toa mifano inayohusiana na jambo kuu, si mambo madogo. Hakikisha kwamba wasikilizaji wako hawakumbuki tu mfano, bali pia wanakumbuka jambo unalofundisha.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki