Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • it uku. 431
  • Kerubi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kerubi
  • Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • “Viumbe Hai Wanne Wenye Nyuso Nne” Ni Nani?
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
  • Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha Kimbingu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Pata Habari Zaidi
Ufahamu wa Kina wa Maandiko
it uku. 431

KERUBI

1. (kerubi). Malaika wa cheo cha juu akiwa na majukumu maalumu, tofauti na yale ya maserafi. Wanatajwa mara 92 katika Biblia, na kwa mara ya kwanza wanatajwa kwenye Mwanzo 3:24; baada ya Mungu kumfukuza Adamu na Hawa kutoka kwenye bustani ya Edeni, makerubi (Kiebr., keru·vimʹ) waliwekwa Mashariki mwa mwingilio kukiwa na upanga unaowaka “ili kuilinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.” Haijulikani ikiwa makerubi waliowekwa hapo walikuwa zaidi ya wawili.

Mifano iliyowakilisha makerubi ilikuwa kati ya vitu vilivyowekwa kwenye hema la ibada lililotengenezwa nyikani. Makerubi wawili waliotengenezwa kwa dhahabu walisimamishwa juu ya miisho ya kifuniko cha Sanduku. Walikuwa wakiangaliana wakiwa wameinama kuelekea kifuniko kama ishara ya ibada. Kila mmoja alikuwa na mabawa mawili yaliyokunjuliwa juu na katikati ya kifuniko katika njia ya kukinga na kulinda. (Kut 25:10-21; 37:7-9) Pia, sehemu ya ndani ya vitambaa vilivyofunika hema la ibada na pazia lililotenganisha Patakatifu na Patakatifu Zaidi vTilitariziwa michoro ya makerubi.​—Kut 26:1, 31; 36:8, 35.

Hayo hayakuwa maumbo ya ajabu yaliyoundwa kwa kufuata picha za kutisha za viumbe wenye mabawa walioabudiwa na mataifa ya kipagani yaliyowazunguka, kama vile wengine wanavyodai. Kulingana na ushuhuda unaokubalika wa tamaduni za kale za Kiyahudi (Biblia haizungumzii jambo hili), makerubi hao walikuwa na umbo la binadamu. Walikuwa kazi bora zaidi ya sanaa, wakiwakilisha malaika wenye utukufu, na walitengenezwa kwa “mkifuata kikamili kielelezo” ambacho Musa alipokea kutoka kwa Yehova mwenyewe. (Kut 25:9) Mtume Paulo anawaelezea kuwa “makerubi wenye utukufu waliokifunika kile kifuniko cha upatanisho.” (Ebr 9:5) Makerubi hao walihusianishwa na uwepo wa Yehova: “Nitakutokea hapo na kuzungumza nawe kutoka juu ya kifuniko hicho. Kutoka katikati ya hao makerubi wawili walio juu ya sanduku la Ushahidi.” (Kut 25:22; Hes 7:89) Hivyo, ilisemwa kwamba Yehova ‘anaketi akiwa mfalme juu ya [au, katikati ya] makerubi.’ (1Sa 4:4; 2Sa 6:2; 2Fa 19:15; 1Nya 13:6; Zb 80:1; 99:1; Isa 37:16) Kwa njia ya kielelezo, makerubi walitumikia kama“mfano wa lile gari” la Yehova ambalo analiendesha (1Nya 28:18), na mabawa ya makerubi yalitoa ulinzi wenye kukinga na kasi katika safari. Hivyo, katika wimbo wake, Daudi alieleza kasi ambayo Yehova alikuja nayo ili kumsaidia, kana kwamba “alipanda juu ya kerubi, akaja akiruka . . . juu ya mabawa ya kiumbe wa roho.”​—2Sa 22:11; Zb 18:10.

Mpango ulioainishwa wa ujenzi wa hekalu lenye utukufu la Sulemani ulikuwa na makerubi wawili kwenye chumba cha ndani zaidi [yaani, Patakatifu Zaidi]. Walitengenezwa kwa mbao za msonobari [Tnn. mti wa mafuta] na kufunikwa kwa dhahabu, kila mmoja akiwa na kimo cha mikono kumi (mita 4.5). Wote walisimama wakitazama Mashariki kwenye usawa wa Kas-Kus ambao inaelekea ulinyooka na kupita katikati ya chumba. Ingawa walisimama umbali wa mikono kumi kutoka kwa mmoja na mwenzake, bawa moja la kila kerubi liligusa ncha ya bawa lililokunjuliwa la yule kerubi mwingine katikati ya chumba, yakifunika sanduku la agano na fito zake ambazo zilikuwa chini ya sanduku. Bawa la pili la kerubi mmoja liligusa ukuta wa Kaskazini na la yule mwingine ukuta wa Kusini. Hivyo basi, mabawa ya makerubi hao yalifunika na upana wa mikono 20 wa chumba. (Ona HEKALU.) Pia, michongo ya maumbo ya makerubi iliyofunikwa kwa dhahabu ilipamba kuta na milango ya hekalu. Vivyo hivyo, makerubi walirembesha kuta za pembeni za magari ya shaba ya kubebea maji. (1Fa 6:23-35; 7:29-36; 8:6, 7; 1Nya 28:18; 2Nya 3:7, 10-14; 5:7, 8) Katika njia hiyohiyo, makerubi waliochongwa walirembesha kuta na milango ya hekalu ambalo Ezekieli aliona kwenye maono.​—Eze 41:17-20, 23-25.

Ezekieli pia anataja maono kadhaa ambapo makerubi wa mfano wenye mwonekano usio wa kawaida walionekana. Baada ya kuwarejelea kama “viumbe hai” (Eze 1:5-28), baadaye Ezekieli anawatambulisha kuwa ni “makerubi.” (Eze 9:3; 10:1-22; 11:22) Katika maono hayo ya kustaajabisha, makerubi wanahusianishwa kwa ukaribu na utukufu wa kibinafsi wa Yehova na mara zote wanatajwa wakimhudumia.

Kwenye kitabu chake cha unabii, Ezekieli aliambiwa “[amwimbie] mfalme wa Tiro wimbo wa huzuni,” ambapo anamwita mfalme huyo kerubi aliyefunikwa na utukufu ambaye hapo awali alikuwa “katika Edeni, bustani ya Mungu,” lakini ambaye aliachwa mtupu na kufanywa kama mavumbi juu ya ardhi. “Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova anasema hivi: . . . ‘Nilikuweka kuwa kerubi anayefunika aliyetiwa mafuta. Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu, nawe ulitembea-tembea kati ya mawe yenye moto. Hukuwa na kosa katika njia zako tangu siku uliyoumbwa mpaka uovu ulipopatikana ndani yako. . . . Nitakufukuza kutoka kwenye mlima wa Mungu kama kitu kilicho najisi na kukuangamiza, . . . ewe kerubi unayefunika [“Ee kerubi mlinzi,” NBT].’”​—Eze 28:11-19.

2. Jiji lililokuwa Babiloni ambalo kutoka kwalo baadhi ya wahamishwa walirudi Yerusalemu mwaka wa 537 K.W.K.; hawakuweza kutambua koo zao na hivyo basi halishindwa kuthibitisha ikiwa walikuwa Waisraeli.​—Ezr 2:59; Ne 7:61.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki