Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 6/1 kur. 5-8
  • Namna Historia Ilivyoandikwa Karne Nyingi Mbele

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Namna Historia Ilivyoandikwa Karne Nyingi Mbele
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • ‘TIRO UTAKUWA MAHALI PA KUTANDAZIA NYAVU ZA WAVUVI’
  • UMEDI NA UAJEMI PAMOJA NA UGIRIKI WATAFUATA BABELI
  • HISTORIA KARNE SITA MBELE
  • Neno la Yehova Ni Hakika!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Tiro—Ulikuwa Mji Wenye Hila
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Unabii Mwingi Uliotimizwa
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
  • Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 5
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 6/1 kur. 5-8

Namna Historia Ilivyoandikwa Karne Nyingi Mbele

UNAONAJE juu ya uwezekano wa mtu fulani kuandika historia kimbele? Wengi wanasisitiza kwamba jambo kama hilo haliwezekani, nao wanatupilia mbali jambo hilo bila kufanya uchunguzi zaidi.

Lakini fikiria jambo hilo kidogo: Je! kukanusha kwa vivi hivi tu kwa watu wenye mashaka kunaondoa uwezekano wa utabiri wa kweli? Bila shaka haingekuwa hekima kukata shauri hivyo haraka-haraka. Pengine papo hapo nyumbani kwako una ushuhuda wa historia iliyoandikwa karne nyingi mbele. Namna gani hivyo?

Labda una nakala ya Biblia Takatifu, ambayo mamia ya mamilioni ya watu ulimwenguni pote huiona kuwa neno lililoongozwa na Mungu. (2 Tim. 3:16) Maandiko hayo yamejaa unabii wa matukio yaliyotukia mamia ya miaka baada ya kutabiriwa. Ebu na tuchunguze mifano kadha.

‘TIRO UTAKUWA MAHALI PA KUTANDAZIA NYAVU ZA WAVUVI’

Mfano ulio sahihi ajabu wa unabii wa Biblia unahusu Tiro mji wa bandarini wa nchi ya kale ya Foiniki. Mji huu ulikua ukawa mkubwa sana kwa hasara ya watu wengi. Ulikuwa na viwanda vya kutengenezea vitu vya chuma, vioo na rangi ya zambarau, makao ya biashara ya misafara iliyokuwa ikipitia juu ya nchi kavu, ghala kubwa la bidhaa zilizoingia na kutoka humo. Wafanya biashara na wachuuzi wake walijivuna kwamba walikuwa wana wa wafalme na wakuu. (Isa. 23:8) Pindi moja kulikuwako uhusiano wa kirafiki kati ya Tiro na Israeli. Lakini haukuendelea, kwa sababu mwishowe Tiro ulijiunga na mataifa adui ya Israeli. Kwa sababu ya kutendea hila Israeli, Mungu aliongoza manabii wake Isaya, Yeremia, Ezekieli na wengine watabiri kwamba msiba ungeipata bandari hii ya Foiniki. Kwa mfano, tunasoma hivi:

“Bwana [Yehova] asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi kupigana nawe, kama bahari iinuavyo mawimbi yake. Nao wataziharibu kuta za Tiro, na kuibomoa minara yake; tena nitakwangua hata mavumbi yake yamtoke, na kumfanya kuwa jabali tupu. Naye atakuwa mahali pa kutandazia nyavu za wavuvi kati ya bahari; . . . Tazama, mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, atakuja juu ya Tiro toka kaskazini, pamoja na farasi, na watu wengi. Nami nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za wavuvi; hutajengwa tena; maana mimi, [Yehova], nimenena hili, asema Bwana [Yehova].”​—Eze. 26:3-5, 7, 14.

Historia ya ulimwengu inaripoti kwamba Nebukadreza alianza mazingiwa ya Tiro muda fulani baada ya kuharibu Yerusalemu na hekalu la ibada ya Yehova katika mwaka 607 K.W.K. Mwanahistoria wa Kiyahudi Yosefo, akitumia historia ya kila mwaka ya matukio na historia nyingine iliyoandikwa mapema ya Kifoiniki, anasema kwamba mazingiwa ya Tiro na Nebukadreza yalichukua muda wa miaka kumi na mitatu. Biblia inaonyesha kwamba majeshi ya Nebukadreza yaliletea Tiro uharibifu mkubwa.​—Eze. 26:8-11.

Tiro ulirudia hali ya kawaida baada ya pigo hilo la Babeli. Hata hivyo, karne nyingi baadaye, majeshi ya Ugiriki chini ya Aleksanda Mkuu yaliinuka juu ya Tiro, ambao wakati huu ulikuwa juu ya kisiwa yapata nusu maili (kilometres 0.8) kutoka bara. Wakaaji walipokataa kujitoa kwa masharti ya Aleksanda, yeye alighadhibika (alipatwa na hasira) sana akaamuru watu wake wakwangue magofu ya mji wa (zamani wa Tiro) wa barani na kuyatupa baharini, hivyo ikajengwa njia ya kufikia ule mji wa kisiwani. Kisha vita ya baharini ikatokea ambayo ilishindwa na majeshi ya Aleksanda. Baada ya mazingiwa ya miezi saba majeshi ya Aleksanda yaliteka mji huo wa kisiwani. Wakaaji wake walipoleta upinzani mkali sana, mji uliteketezwa kwa moto. Ikawa kama vile nabii mwingine, Zekaria, alivyokuwa ametabiri: “Naye mwenyewe atateketezwa kwa moto.”​—Zek. 9:4.

Ijapokuwa karne zilizofuata Tiro uliendelea kujaribu kurudia hali yake ya mbeleni, ulianguka-anguka mbele ya majeshi ya adui, kama vile nabii wa Mungu alivyokuwa ametabiri. (Eze. 26:3) Tiro ambao ulikuwa mojawapo wa mamlaka kuu za baharini za ulimwengu wa kale uko katika hali gani leo? Mahali penyewe, pana magofu na bandari ndogo, iitwayo Souri. Nina Jidejian, katika kitabu chake Tyre Through the Ages (Tiro Baada ya Kupita Vizazi Vingi) (1960), anasema hivi: “Leo bandari imekuwa kituo cha merikebu za kuvuvia samaki na mahali pa kutandazia nyavu [za wavuvi],” sawasawa na ilivyotabiriwa kupitia kwa Ezekieli.​—Eze. 26:5, 14.

UMEDI NA UAJEMI PAMOJA NA UGIRIKI WATAFUATA BABELI

Katika karne ya sita K.W.K., wakati Babeli ilipokuwa ikiongoza ikiwa mamlaka inayotawala ya ulimwengu, nabii Danieli alipata ndoto ya njozi (maono) yenye kushangaza iliyotia ndani wanyama wawili wa mfano. Wa kwanza alikuwa kondoo mume mwenye pembe mbili. “Na pembe zile zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.” (Dan. 8:3) Kondoo mume huyu alifananisha nini? Malaika alimweleza Danieli hivi: “Yule uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi.”​—Dan. 8:20.

Hapa Danieli alipewa kwa jina mamlaka ya ulimwengu ambayo ingefuata Babeli. Kupatana na mambo yote haya, Babeli ulianguka kwa Umedi na Uajemi. Wamedi (pembe iliyo ndogo) walikuwa wenye nguvu zaidi hapo mwanzoni na Waajemi waliinuka hapo baadaye (pembe ndefu iliyotokea baadaye).

Namna gani juu ya mnyama wa pili wa njozi hii? Danieli anatuambia kwamba alikuwa “beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.”​—Dan. 8:5.

Beberu (mbuzi mume) huyu anafanya vita na yule kondoo mume, na kumshinda. (Dan. 8:6, 7) Kisha jambo gani linatukia. Danieli anaendelea kusema hivi: “Alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ikavunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.”​—Dan. 8:8.

Alipouliza malaika maana ya sehemu hii ya njozi yake ya mfano, Danieli alipata jibu hili:

“Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa [Ugiriki]; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza. Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.”​—Dan. 8:21, 22.

Hapa imetabiriwa kwamba Umedi na Uajemi zingefuatwa na Ugiriki katika mamlaka ya ulimwengu.

Namna gani juu ya “pembe kubwa” ya yule mbuzi mume ambayo ilivunjika na badala yake zikatokea pembe nyingine nne? Kama ilivyoonyeshwa katika maelezo ya malaika, ile pembe kubwa ilifananisha “mfalme wa kwanza” wa Ugiriki ikiwa mamlaka ya ulimwengu. Naye alikuwa Aleksanda Mkuu. Linalopendeza ni kwamba, baada ya Aleksanda kufa, muda si muda milki yake iligawanywa mara nne kati ya majemadari wake wanne, ‘kuelekea pepo nne za mbinguni,’ kama ilivyotabiriwa.​—Dan. 8:8.

Kulingana na Yosefo, Aleksanda alionyeshwa unabii huu alipokuja karibu na Yerusalemu Tunasoma hivi: “Alipoonyeshwa kitabu cha Danieli, ambapo yeye [Danieli] alikuwa ametabiri kwamba mmojawapo wa Wagiriki angeharibu milki ya Waajemi, aliamini [kuwa] ni yeye aliyemaanishwa; na kwa sababu ya furaha yake aliruhusu makutano waende kwa wakati huo, lakini siku iliyofuata aliwaita mbele zake tena akawaambia waombe zawadi zo zote wangetaka.”​—Antiguities of the Jews, Kitabu cha XI, sura VIII, fungu la 5.

Kwa hiyo, katika mambo haya machache yanayoeleza njozi ya unabii, kitabu cha Biblia cha Danieli kilitoa historia zaidi ya miaka 200 mbele. Nacho kitabu icho hicho cha Biblia kinafikia hata kwenye wakati mrefu ujao. Namna gani hivyo?

HISTORIA KARNE SITA MBELE

Unabii ulio wa pekee unaopatikana katika Danieli, sura ya 9, unatoa mambo mengi ya historia zaidi ya miaka mia sita mbele. Utabiri huu unataja kwamba “Masihi aliye mkuu” angetokea “majuma sitini na tisa [ya miaka] . . . tangu kuwekwa kwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu,” na kwamba, muda mfupi baadaye, Yerusalemu na hekalu lake ungeharibwa. (Dan. 9:24-27) Hii ilitimizwaje?

Amri ya kutengeneza na kujenga upya Yerusalemu ilitolewa na Mfalme Artashasta Longimano Mwajemi wakati wa mwaka wa ishirini (20) wa utawala wake. Amri hiyo ilianza kufanya kazi wakati wa vuli wa mwaka huo, ambao ulikuwa 455 K.W.K. Tukihesabu majuma sitini na tisa (69) ya miaka (kila “juma” moja likiwa na urefu wa miaka saba), au miaka 483, tangu 455 K.W.K., inatuleta kwenye mwaka 29 W.K. Kulingana na habari ya Maandiko, huo ndio mwaka hasa ambao Yesu wa Nazareti alikuja na kujitoa kuwa Masihi, wakati wa ubatizo wake katika Mto Yordani.​—Luka 3:21-23; 4:16-21.

Utabiri uu huu unasema kwamba Masihi “atakatiliwa mbali . . . [katika] nusu ya juma hiyo [ya sabini].” Kwa kupatana kabisa Yesu alikufa Siku ya Sikukuu ya Kupitwa katika wakati wa masika wa mwaka 33 W.K., nusu barabara ya ‘juma la miaka,’ au miaka mitatu na nusu, baada ya kazi yake ya Kimasihi kuanza wakati wa ubatizo wake.​—Mt. 26:2; Yohana 13:1, 2.

Kwa habari ya uharibifu wa Yerusalemu, unabii huo ulisema hivi kuhusu kizazi ambacho Masihi angetokea na kukatiliwa mbali katika mauti: “Na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.” (Dan. 9:26) Siku tano kabla ya kifo chake Yesu alitoa maelezo zaidi juu ya hilo, maana twasoma hivi:

“Alipofika karibu [na Yerusalemu] aliuona mji, akaulilia, akisema, Laiti ungalijua, hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani! lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.”​—Luka 19:41-44.

Kwa habari ya ‘kujenga boma’ kulikotabiriwa, Yosefo anaripoti kwamba, wakati wa uasi wa Wayahudi, Jemadari Tito wa Kirumi alisisitiza kujengwa kwa ukuta kuzunguka Yerusalemu. Askari wake waling’oa miti mashambani na kwa siku tatu peke yake wakajenga boma lililozunguka mji la miti iliyochongwa lenye urefu wa karibu maili tano (kilometres 8). Katika maangamizi yaliyofuata, 1,100,000 ya “watoto” wa Yerusalemu waliangamia. Kwa habari ya namna utabiri huu ulivyotimizwa kwa ukamilifu, minara mitatu tu na sehemu ndogo ya ukuta wa upande wa magharibi ndiyo iliyobaki ikiwa imesimama. Josefo anaandika hivi: “Maboma mengine yote yaliyozunguka Mji yaliangushwa na kuwa tambarare na nchi hata kwamba mtu ye yote ambaye angetembelea mahali hapo asingeamini kwamba palikaliwa na watu wakati mmoja.”

Uharibifu huu wa Yerusalemu ulitukia katika mwaka 70 W.K., miaka 605 baada ya Danieli kuandika kitabu chake cha Biblia (yapata mwaka 536 K.W.K.). Lo! namna kuchunguza utimizo wa unabii wa Biblia ulioandikwa karne nyingi mbele kunavyoongezea imani nguvu! Walakini utabiri wa Biblia hauhusu tu wakati wa zamani uliopita. Mwingi wake unapata utimizo wa ajabu leo, nao unaonyesha namna wewe unavyoweza kufurahia wakati ujao. Juu ya hili tazama Mnara wa Mlinzi wa Desemba 15, 1978, kur. 17-20.

[Mchoro katika ukurasa wa 7]

(For Fully formatted text, see publication)

“MAJUMA SABINI”

Danieli 9:24-27

455 K.W.K. 33 W.K. 70 W.K.

(masika)

29 W.K. 36 W.K.

Majuma 69 ya Miaka “Juma” la 70

(=Miaka 483)

Yesu

Atiwa Mafuta

Mwaka wa 20

wa Artashasta Yesu Yerusalemu

“Akatiliwa Mbali” Waharibiwa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki