Ni Nani Waliokuwa Waonaji?
Samweli wa Kwanza 9:9 husomwa hivi: “Mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.” Maneno haya yaweza kuonyesha kwamba baada ya manabii kupata kujulikana sana kuanzia na siku za Samweli na kuendelea, neno “Mwonaji” lilikuja kubadilishwa na neno “Nabii” likachukua mahali pake. Waonaji walipata uongozi wa kimungu ‘waone’ hali ya mambo, yaani wafahamu mapenzi ya kimungu. Macho ya mwonaji yalifunuliwa yaone au yafahamu mambo yaliyofichwa watu wengine kwa ujumla. Kwa hiyo, aliendewa atoe shauri katika kushughulika na magumu.