Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 1/1 kur. 3-4
  • Wapanda-Farasi wa Kifumbo wa Kitabu cha Ufunuo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wapanda-Farasi wa Kifumbo wa Kitabu cha Ufunuo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Kulifumbua Fumbo la Wapanda-Farasi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Wapanda Farasi Wanne​—Jinsi Wanavyokuhusu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Wapanda Farasi Wanne​—Jinsi Wanavyokuhusu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 1/1 kur. 3-4

Wapanda-Farasi wa Kifumbo wa Kitabu cha Ufunuo

NATAZAMA kwa msisimuko wakati farasi anapopigisha miguu chini akienda mbio kwenye mteremko wenye mawe-mawe. Aliyempanda anaonekana amezoea kupita katika sehemu hizo ngumu-ngumu na amejibana bila kubanduka kwenye matandiko ya farasi huyo kama kwamba mwili wake ni mmoja na ule wa mnyama huyo mwenye kututuma akipiga shoti.

Hakika kumtazama mpandaji anayejua sana kuendesha farasi kunasisimua sana, iwe ni katika uwanja wa kufugia ng’ombe wa miinuko ya Australia au kule kwenye nyika za Amerika. Wenye kutazamisha jinsi iyo hiyo ni upendezi mwingi wa gwaride la farasi na wapandaji waliozoezwa sana.

Wapanda-farasi hao na miendo yao wanatuacha katika mshangao. Lakini, farasi na wapandaji walioshuhudiwa na mwandikaji wa Ufunuo ni wenye kusisimua kuwatazama! Ni wa fumbo na pia wa kutisha. Wapanda-farasi hao wamejulikana kote kote kuwa Wapanda-farasi wa Ufunuo.

Wazia kwamba sasa wapanda-farasi wanne wanakuja mbio kwa kishindo wakielekea mahali ulipo, mmoja hata akipunga-punga upanga! Ebu tazama rangi ya farasi wanaowaendesha. Kila mmoja ni tofauti. Farasi mmoja ni mweupe, mwingine mwekundu, mwingine mweusi, na kuna mwingine mwenye rangi ya ugonjwa-ugonjwa iliyo mchanganyiko wa kijani na manjano. Hakika wanaonekana wa ajabu-ajabu na wa kifumbo!

Fuatana na masimulizi yenye kwenda kasi kuhusu yaliyoonwa na mwandikaji wa Biblia, mtume Yohana. Yeye anasema: “Ndipo nikaona farasi mweupe, na mwenye kumpanda alichukua uta. Alipewa taji, naye akaendelea kuendesha akiwa mshindi ili akashinde. . . . Na farasi mwingine akatokea, wa rangi iliyo nyekundu-nyangavu, na mwenye kumpanda alipewa uwezo wa kuondoa amani duniani, na kufanya watu wachinjane; yeye alipewa upanga mkubwa. . . . Na kule nikaona farasi mweusi, na mwendeshaji wake alikuwa na jozi ya mizani katika mkono wake, nami nikasikia sauti . . . ikisema, ‘Ngano ya kisaga kimoja kwa [mshahara wa siku moja], na shayiri ya visaga vitatu kwa [mshahara wa siku moja] ‘ . . . Na kule nikaona farasi wa rangi ya majivu, na jina la mwendeshaji wake lilikuwa Kifo, na Hadesi ilimfuata. Wakapewa uwezo juu ya robo moja ya dunia, ili waue watu kwa upanga, njaa, kifo, na wanyama-mwitu wa dunia.”​—Ufunuo 6:2-8, An American Translation.

Tangu njozi hiyo ilipoandikwa mara ya kwanza, maana yake imekuwa isiyoeleweka na wasomaji wengi sana. Ni mambo gani yanayofananishwa na farasi na waendeshaji wao wa kifumbo? Uendeshaji wao ulianza wakati gani? Je, uendeshaji wao una uhusiano wo wote na maisha leo? Maelezo ya namna nyingi yametolewa juu ya mambo yanayoweza kuwa yanafananishwa na farasi hao na waendeshaji wao, na juu ya wakati uendeshaji wao unapotukia.

Utofautiano ulio mkubwa zaidi unapatikana katika fasiri zinazohusu yule farasi mweupe na mwendeshaji wake. Kwa mfano, kitabu New Catholic Encyclopedia kinaeleza kwamba yule farasi mweupe anafananisha ‘ama ushindi wa gospeli ama wa ukoloni.’

Katika kitabu Daniel and the Revelation, Uriah Smith anatoa fasiri hii: “Farasi mweupe . . . ni mfano unaofaa wa shangwe za ushindi za gospeli katika karne ya kwanza . . . Weupe wa farasi unamaanisha utakato wa imani katika kipindi hicho.”

The Expositor’s Bible inasema: “Chini ya yule mwendeshaji wa kwanza, jambo tunalojulishwa si utu wa Kristo bali ni kuksudi lake katika hatua ya mwanzo kabisa ya mwendo walo wenye ushindi, na tunapewa ahadi ya kwamba kusudi hilo litapata ushindi wakati ujao. . . . Tunajifunza kwamba kusudi hilo limo ulimwenguni, kwamba ufalme huo umo katikati yetu, na kwamba wale wanaoupinga watapatwa na ushinde mkubwa.” Lakini, Woodrow Kroll, wa shirika la Hazina ya Wayahudi Wakristo, anatoa maoni ya kwamba mpandaji wa yule farasi mweupe ni yule mpinga Kristo.

Wengine wamedokeza kwamba kuna farasi watano na wapandaji watano, si wanne tu. Kwa hiyo tunaweza kujuaje fasiri iliyo sahihi kati ya hizo nyingi? Tunaweza kuwaje na hakika kwamba kuna ufahamu ulio sahihi? Wapanda-farasa hao wa kifumbo wa kitabu cha Ufunuo ni akina nani hasa, na ni wakati gani uendeshaji wao ulipoanza?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki