Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 4/1 uku. 30
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Habari Zinazolingana
  • Dada Waliokuwa Makahaba
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
  • Sehemu ya 17: 1530 na kuendelea —Uprotestanti—Je! Ni Marekebisho?
    Amkeni!—1990
  • Yehova Achomoa Upanga Wake Kutoka Ala!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Ufalme Bandia Watokea
    “Ufalme Wako Uje”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 4/1 uku. 30

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

◼ Kwa nini Mnara wa Mlinzi wa Septemba 15, 1988, ulionyesha kwamba Uprotestanti umejitia unajisi mwingi kuliko hata Ukatoliki wa Kiroma?

Jambo hilo lilisemwa kwa sababu linafaana na unabii na mambo ya uhakika. Katika kitabu cha Ezekieli sura ya 23, hao Ohola na Oholiba wa kitamathali walielezwa kuwa dada wenye ukosefu wa adili. Ufalme wa Israeli wa makabila kumi uliwakilishwa na Ohola, hali Oholiba alimaanisha ufalme wa Yuda wa makabila mawili. Katika kuzungumzia wanawake hao wa ufananisho, Mnara wa Mlinzi wa Septemba 15, 1988, ulisema hivi katika ukurasa 21:

“Kwa sababu ya kufuatia mwendo wenye dhambi kuliko ule wa dada yake, Oholiba (Yuda) alipatwa na afa la kitaifa mikononi mwa Wababuloni katika 607 K.W.K. Watoto wake walianguka kwa upanga au wakaongozwa waende zao wakiwa mateka, naye akafedheheshwa miongoni mwa mataifa. Kama vile Ohola na Oholiba, Jumuiya ya Wakristo inafanya uzinzi wa kiroho, jambo ambalo ni dhambi machoni pa Mungu ambaye jumuiya hiyo inadai kumwabudu. Uprotestanti, ulio na madhehebu nyingi, umejitia unajisi pamoja na mamlaka za kibiashara na kisiasa za ulimwengu kwa kadiri kubwa kuliko hata dada yao mkubwa zaidi, Ukatoliki wa Kiroma. Hivyo, Yehova atahakikisha kwamba Jumuiya ya Wakristo itaharibiwa yote.”

Kuanza na Baraza la Nikaya katika 325 K.W.K., Mmaliki Konstantino alichanganya kidhehebu cha kipagani cha serikali ya Kiroma pamoja na Ukristo wa uasi-imani na akawa kichwa cha Kanisa Katoliki jipya. Hivyo Kanisa Katoliki la Kiroma linaweza kuona kuwa lilianza kuwako kule nyuma kwenye karne ya nne ya Wakati wa Kawaida wetu. Uprotestanti ulianza katika yale Mageuzo Makubwa ya Kidini ya karne ya 16. Kwa sababu hiyo, kwa kuwa Ohola (Israeli) alikuwa na umri mkubwa kuliko Oholiba (Yuda), kwa kufaa Mnara wa Mlinzi uliita Ukatoliki wa Kiroma dada mkubwa wa Uprotestanti.

Hata hivyo, kwa nini inaweza kusemwa kwamba “Uprotestanti . . . umejitia unajisi pamoja na mamlaka za kibiashara na kisiasa za ulimwengu kwa kadiri kubwa kuliko hata dada (umbu) yao mkubwa zaidi, Ukatoliki wa Kiroma”? Ni kwa sababu mambo ya uhakika yanalingana na unabii huo, unaotaarifu hivi: “Na umbu lake, Oholiba, akayaona hayo, walakini alizidi kuharibika kuliko yeye, na kwa kupendelea kwake [unyege wake, NW], na kwa uzinzi wake, uliokuwa mwingi kuliko uzinzi wa umbu lake.”​—Ezekieli 23:11.

Zikiwa sehemu za Babuloni Mkubwa, ile milki ya ulimwengu ya dini bandia, Ukatoliki na Uprotestanti zimehusika kwa kina kirefu pamoja na wanabiashara na wanasiasa wa ulimwengu huu. (Ufunuo 17:1-6; 18:1-19) Ni kweli, huenda dhehebu moja la Kiprotestanti likawa na uvutano kidogo kuliko Kanisa Katoliki la Kiroma lenye nguvu nyingi. Lakini makanisa yale mengi ya Kiprotestanti yakiwa yameunganishwa pamoja yana uwezo na uvutano mwingi sana kuliko lile Kanisa Katoliki moja. Mathalani, Uprotestanti hutokeza uvutano mwingi katika nchi fulani mashuhuri zenye viwanda, huku makasisi fulani Waprotestanti wakitafuta cheo cha juu cha kisiasa. Kwa hiyo hii ni njia moja ambavyo Uprotestanti, ukiwa na madhehebu yao mengi, umejichafua hata kuliko Ukatoliki.

Hata hivyo, kuna njia nyingine ambavyo Uprotestanti ‘umejizoeza tamaa yenye nyege kwa uharibifu mwingi zaidi’ na unalaumika kuliko Ukatoliki. Jinsi gani? Basi, yale Mageuzo Makuu ya Kidini yaliupa Uprotestanti angalau tumaini na tazamio la kupata nuru kubwa zaidi ya kiroho. Kwa uhakika, wanamageuzo fulani walichukua hatua kubwa na za moyo mweupe kwa habari hiyo. Lakini kila jambo liliposemwa na kufanywa, mafundisho yasiyo ya Kimaandiko kama vile Utatu, kutokufa kwa nafsi ya kibinadamu, na moto wa mateso yaliendelea bila kubadilika miongoni mwa Waprotestanti. Kama vile Wakatoliki, wao pia wamekuwa na hatia ya kujihusisha katika ibada ya kiumbe na ya kuweka mapokeo ya wanadamu mahali pa ukweli wa Kibiblia.​—Mathayo 15:1-9; 23:9, 10.

Jambo la kupendeza katika habari hii ni lile lililotaarifiwa katika Vindication, Kitabu cha Kwanza, kule nyuma katika mwaka 1931. Katika ukurasa wa 309, kichapo hicho cha Mnara wa Mlinzi (ambacho sasa hakimo akibani) kilisema hivi kuhusu Ezekieli 23:11-13: “‘Dini iliyopangwa kitengenezo’ ya Uprotestanti iliona jinsi Ukatoliki wa Kiroma ulikuwa umejitia unajisi pamoja na mamlaka za kibiashara na kisiasa za ulimwengu huu, na ikasema mengi dhidi ya Wakatoliki kwa sababu hiyo; lakini ndipo Uprotestanti ulipoenda na moja kwa moja ukafanya hivyo hivyo, na hata vibaya zaidi. . . . Zote mbili zimechukua mwendo ule ule mmoja; lakini Uprotestanti umekuwa na nuru nyingi kuliko Uroma, na kwa hiyo ndio wa kulaumika zaidi.”

[Picha kutoka ukurasa wa 30]

Mmaliki Konstantino alichanganya Ukristo wenye uasi-imani pamoja na kidhehebu cha kipagani cha serikali ya Kiroma, hivyo akawa kichwa cha Kanisa Katoliki lililo jipya

[Hisani]

Jumba la Mjini la Makumbusho ya Sanaa. Wasia wa Bi F. F. Thompson, 1926.(26229)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki