Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 6/1 kur. 8-9
  • Sikukuu-Kupitwa Iliyo ya Mwisho Kwake Yesu Yakaribia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sikukuu-Kupitwa Iliyo ya Mwisho Kwake Yesu Yakaribia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Sikukuu ya Kupitwa Iliyo ya Mwisho kwa Yesu Yakaribia
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Pasaka ya Mwisho ya Yesu Yakaribia
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • “Siku Hii Itakuwa Ukumbusho Kwenu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Kuzikumbuka Siku za Mwisho za Yesu Duniani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 6/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Sikukuu-Kupitwa Iliyo ya Mwisho Kwake Yesu Yakaribia

JUMANNE, Nisani 11, ikaribiapo, Yesu amaliza kufundisha mitume juu ya Mlima wa Mizeituni. Lo, imekuwa siku yenye mikazo na shughuli kama nini! Sasa, labda akiwa anarudi kwenda Bethania akakae huko usiku huo, awaambia hivi mitume wake: “Nyinyi mwajua kwamba siku mbili kuanzia sasa sikukuu-kupitwa yatukia, na Mwana wa binadamu atatolewa atundikwe.”

Siku inayofuata, Jumatano, Nisani 12, yaonekana Yesu ajitenga kando kwa utulivu ili awe na mitume wake tu. Siku iliyotangulia, alikuwa amewakemea peupe viongozi wa kidini, naye ang’amua kwamba wanatafuta kumwua. Kwa hiyo siku ya Jumatano hajionyeshi waziwazi, kwa kuwa hataki kitu chochote kikatize kuadhimisha kwake Sikukuu-Kupitwa pamoja na mitume wake jioni inayofuata.

Wakati uo huo, makuhani wakuu na wanaume wazee wa watu wamekusanyika katika ua wa kuhani wa juu, Kayafa. Wakiwa na udhia wa kushambuliwa na Yesu siku iliyotangulia, wanafanya mipango ya kumbamba kwa mbinu ya ujanja na kufanya auawe. Na bado wanafuliza kusema hivi: “Si kwenye ule msherehekeo, ili kwamba zahama yoyote isitokee miongoni mwa watu.” Wanawahofu watu, ambao wamwonea Yesu shangwe.

Huku viongozi wa kidini wakitunga kwa uovu njama ya kumwua Yesu, wapokea mgeni. Wao washangazwa na jambo la kwamba ni mmoja wa mitume wa Yesu mwenyewe, Yuda Iskariote, mmoja ambaye Shetani amepanda ndani yake lile wazo bovu la kusaliti Bwana-Mkubwa wake! Wao wapendezwa kama nini Yuda aulizapo hivi: “Nyinyi mtanipa nini nikimsaliti yeye kwenu?” Wao waafikiana kwa mteremo kumlipa vipande 30 vya fedha, bei ya mtumwa kulingana na agano la Sheria ya Musa. Tangu hapo na kuendelea, Yuda atafuta fursa nzuri ya kumsaliti Yesu kwao wakati pasipokuwa na umati wenye kuzunguka.

Nisani 13 yaanza kwenye mshuko-jua wa Jumatano. Yesu alikuwa amewasili kutoka Yeriko siku ya Ijumaa, kwa hiyo huu ndio usiku wa sita na wa mwisho ambao atumia akiwa Bethania. Siku inayofuata, Alhamisi, matayarisho ya mwisho yatahitaji kufanywa kwa ajili ya Sikukuu-Kupitwa, ambayo yaanza kwenye mshuko-jua wakati ambapo ni lazima mwana-kondoo wa Sikukuu-Kupitwa achinjwe halafu achomwe akiwa mzima. Wataadhimisha wapi karamu hiyo, na ni nani atafanya matayarisho?

Yesu hajaandaa maelezo hayo, labda ili kumzuia Yuda asiwapashe habari makuhani wakuu ili waweze kumkamata Yesu wakati wa mwadhimisho wa Sikukuu-Kupitwa. Lakini sasa, labda ikiwa ni mapema alasiri ya Alhamisi, Yesu awatuma Petro na Yohana kutoka Bethania, akisema: “Endeni mkatutayarishie sikukuu-kupitwa ili tule.”

“Wataka tuitayarishe wapi?” wao wauliza.

“Mwingiapo ndani ya jiji,” Yesu aeleza, “mwanamume mmoja mwenye kubeba nyungu ya maji atawalaki. Mfuateni ndani ya nyumba ambamo yeye aingia. Nanyi ni lazima mseme kwa mmiliki-ardhi wa ile nyumba, ‘Mwalimu asema kwako hivi: “Kiko wapi chumba cha mgeni ambamo mimi naweza kula sikukuu-kupitwa pamoja na wanafunzi wangu?”’ Na mwanamume huyo atawaonyesha chumba cha juu kikubwa chenye vifaa. Itayarisheni humo.”

Bila shaka mmiliki-ardhi huyo ni mwanafunzi wa Yesu ambaye labda atazamia ombi la Yesu kutumia nyumba yake kwa pindi hii maalumu. Vyovyote vile, Petro na Yohana wawasilipo katika Yerusalemu, wakuta kila kitu kama vile Yesu alivyotabiri. Kwa hiyo wao wawili wahakikisha kwamba mwana-kondoo yuko tayari na kwamba mipango mingine yote yafanywa ili kutimiza mahitaji ya waadhimishi wale 13 wa Sikukuu-Kupitwa, Yesu na mitume wake 12. Mathayo 26:1-5, 14-19; Marko 14:1, 2, 10-16; Luka 22:1-13; Kutoka 21:32, NW.

◆ Yaonekana Yesu afanya nini Jumatano, na kwa nini?

◆ Ni mkutano gani ambao wafanywa nyumbani kwa kuhani wa juu, na Yuda awazuru viongozi wa kidini kwa kusudi gani?

◆ Yesu atuma nani wakaingie Yerusalemu Alhamisi, na kwa kusudi gani?

◆ Hawa waliotumwa wakuta nini ambacho chafunua tena nguvu za kimwujiza za Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki