Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 8/1 uku. 22
  • “Wenye Furaha ni Wenye Kutafuta Amani”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Wenye Furaha ni Wenye Kutafuta Amani”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Usiruhusu Chochote Kikunyang’anye Tuzo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Mtetezi wa Vita Au Mteteaji wa Amani?
    Amkeni!—2002
  • ‘Tafuteni Sana Amani na Kuifuatia’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Kaza Macho Yako Kwenye Tuzo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 8/1 uku. 22

“Wenye Furaha ni Wenye Kutafuta Amani”

KATIKA 1901 Zawadi ya Nobeli ya Amani, iliyotolewa kwa mara ya kwanza, ilishirikiwa na Jean-Henri Dunant, mwanzilishi wa Msalaba Mwekundu, na mtaalamu wa uchumi Frédéric Passy. Tangu wakati huo imetuzwa mara 69, mara 55 kwa watu tofauti-tofauti 71, wakiwa mmoja mmoja au wakiwa mwungano, na mara 14 kwa vikundi au mashirika 16. Vikundi fulani vimeishinda zaidi ya mara moja, kama vile Halmashauri ya Msalaba Mwekundu wa Kimataifa (1917, 1944, na 1963) na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Ajili ya Wakimbizi (1954 na 1981). Yaonekana kwa sababu ya kukosa mpokezi mwenye kustahiki, halmashauri ya zawadi ya Nobeli ilikataa kutoa tuzo mara 19.

Kama vile mtu angewazia, walio wengi wa washinda zawadi wamekuwa viongozi wa serikali, wanaubalozi, au watu wenye kuhusika na siasa kwa njia nyinginezo. Lakini waandishi wa habari, washiriki wa mabaraza ya hukumu, wanasosholojia, wataalamu wa uchumi, na warekebishi wa hali za kijamii wameipokea pia. Hata wanasayansi, miongoni mwao wakiwamo Linus Pauling katika 1962 na Andrey Sakharov katika 1975, wamepewa heshima hiyo, hata viongozi wa wafanya kazi, mwenye kujulikana sana akiwa ni Lech Walesa katika 1983. Na katika 1970 zawadi hiyo ilipewa kwa bingwa wa ukulima Norman E. Borlaug.

Mwanadini wa kwanza kutuzwa zawadi hiyo alikuwa askofu mkuu wa Lutheri ya Sweden, Nathan Söderblom, aliyechaguliwa katika 1930. Katika 1946 mwanakanisa wa kawaida Mmethodisti na mwevanjeli John R. Mott walishirikiana zawadi hiyo, wakifuatwa katika 1952 na mwanatheolojia na mwanafalsafa Albert Schwitzer na katika 1958 na kasisi Mbelgiji Dominique Georges Pire. Katika 1964 chaguo lilikuwa kiongozi wa haki za kiraia na mhudumu Mbaptisti Martin Luther King, Jr.

Lakini katika miaka ya majuzi, dini imekuwa ikishiriki fungu maarufu zaidi katika jitihada ya ulimwengu ya kufuatia amani. Kupatana na elekeo hilo, watatu kati ya watu tisa wa mwisho kutuzwa Zawadi ya Amani ya Nobeli wamekuwa ni wanadini: Mtawa wa kike Mkatoliki Mama Teresa wa Calcutta katika 1979, askofu Mwanglikana Desmond Tutu wa Afrika Kusini katika 1984, na mwaka uliopita ikawa ni “mfalme-mungu,” Mbuddha wa Tibeti aliyepelekwa uhamishoni, yule Dalai Lama.

Ni kweli kwamba Yesu Kristo alisema hivi: “Wabarikiwa ni wafanya amani.” (Mathayo 5:9, King James Version) Lakini je! jitihada za kidini—ziwe ni za Kikatoliki, Kiprotestanti, Kibuddha, au nyinginezo—za kutumikia kuwa wafanya amani katika ulimwengu huu zitapata mafanikio hatimaye?

Biblia yatuambia kwamba ulimwengu mwovu huu uliopo ambao umetenganishwa na urafiki wa Mungu hautaona kamwe amani yenye kudumu, na huo ni uhakika ambao mhusiko wa kidini katika mambo ya ulimwengu ya kutoa misaada ya ufadhili, ya kijamii, na ya kisasa hauwezi kuubadili. Kwa kuondoa serikali zilizopo na kuuweka mahali pazo Ufalme wake chini ya Kristo Yesu, yule “Mwana-Mfalme wa Amani,” hivi karibuni Muumba mwenyewe atabariki ainabinadamu inayoamini kwa kuipa amani.—Isaya 9:6, 7, NW; 57:21; Zaburi 46:9; Danieli 2:44.

Watu watafutao amani ambao wautambua ukweli huo na ambao wafuatisha maisha zao kwa kigezo hicho watafurahi kweli kweli. Kama vile New World Translation ifasirivyo maneno ya Yesu: “Wenye furaha ni wenye kutafuta amani.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki